FLORA MVUNGI ADAIWA KUTAPELI HELA ZA UPATU - LEKULE

Breaking

12 Jun 2015

FLORA MVUNGI ADAIWA KUTAPELI HELA ZA UPATU

Mwanadada Flora Mvungi anayeendesha maisha yake kwa kuuza nyago kwenye filamu, hivi karibuni aligandwa na skendo ya kutapeli pesa za upatu za dada aliyefahamika kwa jina la Christina ambaye ilikuwa imefika zamu yake ya kupokea.

Sosi wa habari hii alisema kuwa, Flora baada ya kupokea fedha hizo za upatu aliendelea na shughuli zake kama kawaida lakini ilipofika zamu ya Christina kupokea aliingia mitini na kila alipokuwa akipigiwa simu alikuwa hapokei.

“Cha kushangaza sisi ni kundi lakini hata alipokuwa na sherehe yake juzikati hakutualika kisa kikiwa ni hizo hela, sisi tunamsihi kama mchezo umemshinda arudishe tu hela za watu,” alisema sosi aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Flora alitafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia tuhuma hizo ambapo alipopatikana alishangazwa na kitendo cha habari hizo kufika gazetini kisha akakata simu.


Mtangazaji Maimartha Jesse ambaye ndiye mweyekiti wa kikundi hicho alipotafutwa kufafanua madai hayo alisema: “Yaani haya mambo hayawahusu kabisa, ni mambo binafsi nawaomba muachane nayo.”

No comments: