WASTARA: WANASIASA WANATUTUMIA KAMA BIG G TU - LEKULE

Breaking

12 Jun 2015

WASTARA: WANASIASA WANATUTUMIA KAMA BIG G TU

Staa wa filamu za Kibongo Wastara Juma, ameibuka na kusema kuwa wanasiasa wanawatumia wasanii wakiwa na shida zao lakini wakishapata uongozi huwasahau na kuwaona ni wasumbufu pale wanapohitaji msaada.

Akipiga stori  hivi karibuni, Wastara alisema kuwa kwa sasa wao watakuwa lulu kwa wanasiasa na kutumiwa ipasavyo lakini baada ya mchakato wa uchaguzi kuisha wataonwa hawafai, kitendo ambacho si kizuri kwani wanatakiwa kukumbukwa wakati wote.

“Yaani kuna wakati sipendi kabisa siasa na wala sipendi kufungamana na mtu kwa sababu nilichojifunza sisi wasanii tunatumiwa kama Big G tu kwa sasa kwa sababu wana shida, baada ya hapo tutaachwa solemba na hata tutakapohitaji kusaidiwa jambo lenye masilahi kwetu tutaonekana wasumbufu,” alisema Wastara.

No comments: