Utafiti wa DNA unatarajiwa
kuthibitisha kuwa mmoja wa wapiganaji 11 wa Al shabaab waliouawa na
wanajeshi wa Kenya hapo jana alikuwa ni raia wa Uingereza.
Duru za
kijasusi za jeshi la Kenya zinasema kuwa mmoja kati ya watu wawili
wazungu waliouawa anafahamika kama Thomas Evans, 25, ambaye ni raia wa
Uingereza na anayetokea Buckinghamshire.Bwana Evans, alisilimu na kubadili jina lake na kuitwa Abdul Hakim.
Familia yake imeiambia BBC kuwa inasubiri hakikisho kutoka kwa serikali ya Uingereza kuwa ndiye aliyeuawa.
Shambulizi hilo lilitokea jana alfajiri katika kambi ndogo ya kijeshi iliyoko Baure karibu na Lamu ambapo wanajeshi sasa wamethibitisha kuwa waliwauawa watu 11 na kupata bunduki 13 na mizinga mingine tano.
silaha zilizopatikana baada ya kuawa |
Maafisa wa utawala nchini uingereza wanashirikiana na utawala nchini Kenya kubaini haswa ni nani aliyeuawa.
Kwa mujibu wa polisi katika bonde la Thames nchini Uingereza , mamake Thomas bi Sally Evans amenukuliwa akisema kuwa ''yeye na mwanaye Michael wanasubiri thibitisho kutoka kwa duru za polisi''
Awali Familia yake ilikuwa imeilaumu idara ya uhamiaji ya Uingereza kwa kumruhusu kuondoka nchini humo.
Evans alisafiri kuelekea Misri mwaka wa 2011 punde baada ya kunyimwa ruhusa ya kuenda Kenya.
takriban raia 50 wa UK wamejiunga na Al Shabab |
Mnamo mwaka wa 2012 Evans inafahamika alimuarifu mamake kuwa amesafiri hadi Somalia kujiunga na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Takriban raia 50 wa Uingereza wanaaminika kuwa wamejiunga na al-Shabaab nchini Somalia.
Kundi hilo ndilo linalolaumiwa kwa kutekeleza mashambulizi kadha nchini Kenya na pia Somalia.
Iwapo mwili huo utathibitishwa kuwa wa Evans basi itakuwa ndio mara ya kwanza kwa raia wa Uingereza kuuawa cnhini kenya akipigania kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
No comments:
Post a Comment