ADEBAYOR AIPANIA TOTTENHAM - LEKULE

Breaking

22 Jun 2015

ADEBAYOR AIPANIA TOTTENHAM

Baada ya majanga kutokana ana ugomvi na mama na ndugu zake mchezaji mwenye uraia wa taifa la Togo Emmanuel Adebayor ameonyesha kupania kuonyesha makali yake ndani ya klabu yke ya Tottenham msimu ujao utakapoanza.
Adebayor hivi karibuni ameonekana mwenye furaha na kukaa sawa kiakili baada ya malumbano na familia yake kitu kilichoelezwa kuwa ni moja kati ya mambo yaliyomfanya mchezaji huyo kushuka kiwango msimu uliopita kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza.
Adebayor aliyekua anasifika kwa kutingisha nyavu za timu pinzani, Msimu uliopita amefunga magoli mawili tu kati ya mechi 17 alizowahi kucheza.
Pamoja na habari kuenea kwamba klabu ya West Ham inamtaka mchezaji huyo kwa mkopo kwa ajili ya msimu ujao, lakini Adebayor haonyeshi nia ya kukubali ombi hilo bali anatakakusalia ndani ya Tottenham na kuonyesha uwezo wake.

No comments: