MSEMAJI
wa Kambi Rasmi ya Upinzani na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,
ameichachafya serikali akidai imekithiri kwa ahadi hewa ambazo zimekuwa
zikitolewa na Rais Jakaya Kikwete na mawaziri kuhusiana na Kura ya
Maoni ya Katiba Pendekezwa.
Lissu
alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano wa 20 wa Bunge unaoendelea mjini
Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya kambi pinzani kuhusu makadirio
ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Lissu
alisema Rais Kikwete wakati akikabidhiwa katiba pendekezwa aliwaahidi
Watanzania kuwa katiba hiyo ingepigiwa kura ya maoni Aprili 30, mwaka
huu lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.
Alisema
leo ni wiki ya 3 tangu Rais awaahidi Watanzania juu ya upigaji wa kura
ya maoni lakini mpaka sasa haijulikani siku wala tarehe ya kura ya maoni
kutokana na ubabaishaji uliopo ndani ya Serikali.
Lissu
alisema ni dhahiri hakuna uhakika wowote kufanyika kura ya maoni juu ya
katiba mpya kutokana na sheria iliyopo ya kura ya maoni ya mwaka 2015.
Alisema
kwa sasa kuna uhakika wa Rais kuondoka madarakani bila ya katiba mpya
aliyowaahidi Watanzania kupatikana katika kipindi cha takribani miaka
mitano iliyopita.
Mbunge huyo machachari alisisitiza; "Ndani ya utawala wa Rais Kikwete unaonesha dhahiri kuwa ameshindwa kukamilisha mchakato huo pamoja na chama chake CCM.
"Hata
kama tume ya uchaguzi itaweza kukamilisha jukumu lake la kuandikisha
wapiga kura nchi nzima bado hakuna uhakika wa kufanyika kwa kura ya
maoni kutokana na matakwa ya sheria ya kura ya maoni 2015."
Alisema
Sheria hiyo iliweka utaratibu mgumu wa uendeshaji wa kura ya maoni
ambapo kila hatua inayotakiwa kuchukuliwa haiwezekani kuahirishwa kwa
kuongezewa muda.
Aakizungumzia haki za binadamu, Lissu alisema kwa kiasi kikubwa ukiukwaji wa haki za binadamu umeongezeka kwa Watanzania.
Alisema
mauaji na mashambulizi dhidi ya viongozi wa kidini na waumini wao
kufanyiwa ukatili sehemu zao za ibada hakuna mtu yeyote aliyeadhibiwa
katika kesi hizo.
"Serikali
haijatoa taarifa yoyote juu ya wahusika na wauaji wa mashambulio
mbalimbali yaliyofanyika nchini, yakiwemo ya Daud Mwangosi pamoja na
shambulio la Dkt.Ulimboka hadi sasa hayajajulikana hatma yake,"alisema Lissu.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma, Felix Mkosamali alisema
ni aibu kwa nchi katika kura ya maoni kwani sheria yake bado
haitekelezeki na haiwezekani kwa mazingira ya sasa yalivyo inashangaza
waziri wa sheria kutangaza kuwepo kwa kura hiyo.
Mkosamali
alisema hii ni aibu kwa nchi kuendeshwa bila ya kuwa na uhakika nayo
wala kuwa na ratiba au sheria inayoeleweka kwani hata katiba hiyo
ikilazimika kupigiwa kura inakuwa haina umuhimu kwa wananchi wake.
"Kwa
hili serikali imeshafeli tangu mwanzo mchakato huu wa katiba ni
mchakato ambao ukiutafakali unashangaza hasa kwa chama cha CCM
kushauriana na vyama vingine kwani katiba za wenzetu ni nzuri na zenye
mashiko kwa jamii yao,"alisema Mkosamali.
Akizungumzia
Sheria iliyopo sasa nchini, Mkosamali alisema Sheria zinazotekelezwa
nchini ni asilimia 30 mambo mengi yanaendeshwa kiholela bila kufuata
sheria.
Alisema
hali ya watu kutumia sheria mikononi imeweza kuongezeka kutokana na
jamii kutoamini serikali ambapo mara nyingi wanapowafikisha watuhumiwa
polisi wanaachiwa.
No comments:
Post a Comment