Tusker
Lager kupitia kampeni yake ya “Fanya kweli” wiki hii inawaletea wateja
wake shindano la wiki lilopewa jina la “Fanya kweli Kiwanjani”. Shindano
hilo litahusisha baa mbalimbali za mitaani tunapoishi ndani ya jiji la
Dar Es Salaam.
Kampeni
hii ya “Fanya Kweli” imekua na lengo la kuhamasisha watanzania
kujitengenezea maisha mazuri ya baadaye kupitia juhudi zao binafsi
pamoja na msaada wa wadau ambapo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa
kuhamasisha na kubadilisha fikra za watanzania wengi kupitia vipindi na
matamasha yanayolenga kuthamini watanzania wenzetu waliofanikiwa katika
maisha na hivyo kuwapa motisha watu wengine kufuata nyayo zao.
Shindano
hili ambalo litadumu kwa takriban muda wa wiki tano, linatazamia kutoa
zawadi mbalimbali kwa wapenzi wa bia ya Tusker na baa zao wanazozipenda
ambapo zaidi ya baa 50 jijini Dar es salaam zinatarajiwa kushiriki
kikamilifu kwenye shindano hilo.
Kati
ya baa 50 zitagawanywa kwenye makundi ya baa 10 kwa wiki ambapo
zitapewa promo nzito wiki husika kupitia kituo cha redio cha E-fm kwenye
kipindi cha “Ubaoni” kinachorushwa kati ya saa tisa mchana mpaka saa
moja usiku na watangazaji wake mashuhuri, Gardner G. Habash na Seth
wataipa promo kampeni hii nzima pamoja na kuwakumbusha wapenzi wa baa
zinazoshindana kushiriki kwenye kampeni hii.
Watangazaji
hawa pia watagawana baa 5 kati ya 10 zitakazo shindanishwa, kisha
kuwaomba wasikilizaji wao kuchagua baa 1 bora na baa itakayoibuka
mshindi kituo cha radio cha E-fm kitafunga kambi ndani ya baa hiyo na
kuwafanyia sherehe pamoja na kukabidhi zawadi mbalimbali. Watangazaji
hawa pia watatoa maelekezo ya jinsi gani wasikilizaji watakavyoweza
kuzipigia kura baa wazipendazo na pia jinsi ya kushinda zawadi ndogo
ndogo zitakazotolewa kwa wasikilizaji wa kipindi hicho cha redio.
Kupitia
shindano hili, Tusker imedhamiria kusaidia katika kuzitangaza zaidi baa
maarufu za mitaani tunapoishi sambamba na kuibua sifa za huduma nzuri
zitolewazo na baa hizo huku pia ikionekana kama njia ya kuwaongezea
mauzo kwa ujumla.
Kuna
njia mbalimbali ambazo mashabiki wa Fanya kweli kiwanjani wanaweza
kuzitumia katika kuzipigia kura baa wazipendazo ambapo anachotakiwa mtu
kufanya ni kutembelea baa ya mtaani kwake na kunywa bia ya Tusker,
kupiga picha na kisha kuweka picha hizo kwenye kurasa za jamii (Facebook
na Twitter) za Tusker au kusikiliza E-fm kwa maelekezo zaidi.
No comments:
Post a Comment