MKAZI
wa Kijiji cha Ndeleta kilichopo wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, Saria
Kidali (47), amefariki dunia baada ya kunyongwa na shuka alilokuwa
amejifunika wakati akiendesha pikipiki.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana asubuhi wakati Kidali alipokuwa akitoka shambani kwake Nadosoiti.
Kabla
ya kifo hicho, shuka ya mwendesha pikipiki huyo ilinasa kwenye tairi ya
nyuma na shuka hiyo kumbana shingo Kidali hadi alipopoteza maisha baada
ya kudondoka chini.
Kamanda
wa Polisi, Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuitaja pikipiki iliyomuua Kidali kuwa ni aina ya Toyo
yenye namba za usajili T613 BEB.
“Pikipiki
hiyo inasemekana ni mali ya marehemu na taarifa za awali zinaonyesha
chanzo cha kifo hicho ni shuka alilokuwa amevaa kwani lilijizungusha
kwenye tairi na kumnyonga shingo,” alisema Kamanda Fuime.
Pamoja na hayo, alitoa wito kwa waendesha pikipiki kuchukua tahadhari wakati wote ili kuepukana na ajali zinazoweza kuepukika.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo, waliitonya LEKULE kwamba, walipata taarifa
za tukio hilo kutoka kwa abiria wa basi moja la abiria lililokuwa
likitoka wilayani Kiteto kuelekea Arusha.
Mmoja
wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Lazaro Gidion, alisema
marehemu Kidali hakukutwa na majeraha yoyote ingawa shingo yake ilikuwa
imezungukwa na shuka.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndaleta lilikotokea tukio hilo, Ijumaa Bakari,
aliwataka wananchi wa eneo hilo kutovaa shuka wakati wanaendesha
pikipiki kwa kuwa zinaweza kuhatarisha maisha yao
No comments:
Post a Comment