Saudi Arabia haina haki ya kuchukua maamuzi kuhusu
misaada ya kibinadamu inayoelekea Yemen nchi ambayo inakabiliwa na
hujuma ya kijeshi ya watawala wa Riyadh.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya nje ya Iran Hossein Amir-Abdollahian anayeshughulikia masuala ya Kiarabu na Kiafrika.
Ameongeza kuwa hatua ya utawala wa Saudia kuzuia misaada ya
kibinadamu Yemen imepelekea watu katika mikoa 20 nchini humo kukosoa
mahitajio ya dharura. Amir-Abdollahian ameongeza kuwa Iran iko tayari
kutuma misaada katika maeneo yote ya Yemen. Tayari Saudia imeshazuia
ndege kadhaa za Iran zifikishe misaada ya chakula na dawa nchini Yemen.
Hivi sasa meli ya misaada ya Iran inayosheheni chakula na dawa iko
njiani ikielekea Yemen. Iran imeionya Marekani na Saudia kuwa hujuma
yoyote ya kijeshi dhidi ya meli hiyo itaibua moto katika eneo. Ikumbukwe
kuwa Saudia ilianzisha hujuma dhidi ya Yemen mnamo Machi 26 bila ya
idhini ya Umoja wa Mataifa. Lengo la hujuma hiyo ni kuiangusha harakati
ya Ansarullah iliyoko madarakani na kumrejesha rais wa zamani wa nchi
hiyo Abd Rabbuh Mansur Hadi ambaye ni kibaraka wa Saudia.
No comments:
Post a Comment