OFISA
Afya wa Kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Mkola
Vedastus (27), amenusurika kifo baada ya kumwagiwa maharage ya moto
yaliyokuwa jikoni.
Tukio hilo lilitokea juzi wilayani hapa baada ya ofisa huyo kumwagiwa maji hayo na shemeji yake, Anna Makula.
Akizungumza
juzi akiwa Kituo cha Afya cha Igalilimi alipolazwa, Vedastus alisema
alikutwa na mkasa huo jioni wakati anatoka bafuni akiwa amevaa taulo na
ghafla shemeji yake alimmwagia maji hayo.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa ndani na shemeji yake ambaye wamepanga nyumba moja katika mtaa huo.
Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa Kituo cha Afya Igalilimi, Dk. Shija Luis, alisema hali ya mgonjwa huyo bado si nzuri.
“Majeraha
ya mgonjwa ni makubwa, kwa kuwa hadi sasa tunahangaika kuona namna ya
kuokoa maisha yake, majibu ya vipimo yatapatikana baada ya siku tatu
lakini kwa sasa tumempatia huduma ikiwemo kumwongezea maji mwilini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamgisha, alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema bado halijafika ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment