RAZA AWAONYA WAGOMBEA URAIS KUTOTUMIA RUSHWA - LEKULE

Breaking

17 May 2015

RAZA AWAONYA WAGOMBEA URAIS KUTOTUMIA RUSHWA


Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Raza (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Vincent Tiganya.

Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

Raza akiwa na Vincent Tiganya.
MJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Uzini amewaasa viongozi wanaotaka kuwania nyadhifa za ubunge na urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu kuacha kutumia rushwa kuwashawishi wananchi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo asubuhi amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwa macho kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa wabunge na rais kutokushawishiwa kwa fedha watakazokuwa wanapewa na watu wanaojitangaza kutaka kugombea bali wawapuuze.

Alisema kuwa wananchi sasa ni muda wao kuwapima wale wote walioweza kuingia jimboni kwa kipindi cha miaka mitano wakiwa wabunge ama wawakilishi wao kwa yale yote waliyofanya jimboni kwao na si vinginevyo, kwani kama mbunge hakuweza kutimiza ahadi zake, kumrudisha jimboni kwa vile ametoa fedha chumvi na vitenge ni kupoteza haki ya kupiga kura na kuchagua kiongozi bora.

Raza alieleza aliyoweza kuwafanyia wananchi wa jimbo lake ikiwa ni pamoja na kuwajengea miundombinu, kuchangia katika ujenzi wa maabara za shule, kujenga zahanati na hata kuhakikisha kila mwananchi anapunguziwa michango ambayo ilikuwa ikijitokeza kwa wingi kabala ya kipindi chake.

Aidha alitoa ufafanuzi juu ya sakata la kashfa ya fedha za Escrow jinsi lilivyoathiri Zanzibar kwa kukosa misaada kutoka nje na hata kwa wawekezaji, hatua aliyosema kuwa Zanzibar haihusiki na kashfa hiyo, akataka waliohusika na fedha hizo wawajibishwe ili nchi iweze kusonga mbele.

No comments: