MLIPUKO WA BOMU WAUA WATATU KABUL - LEKULE

Breaking

17 May 2015

MLIPUKO WA BOMU WAUA WATATU KABUL


WATU watatu wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine takribani 20 wakijeruhiwa baada ya mlipuko kutokea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Kabul nchini Afghanistan leo.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa mlipuaji wa bomu hilo la kujitolea muhanga alikuwa amelenga wanajeshi wa kimataifa nje ya lango kuu la uwanja huo wa ndege.

Lango hilo hutumika na vikosi vya kijeshi vya kigeni. Kundi la Taliban limethibitisha kuhusika na shambulio hilo katika taarifa yake lililoituma kwa wanahabari.

Shambulizi hilo linafanyika ikiwa ni siku tatu baada ya mwanamgambo mmoja wa Taliban kuwaua watu 14 wakiwemo raia tisa wa kigeni katika hoteli moja mjini humo.

No comments: