Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare
ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza
amepinduliwa madarakani.
Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua
hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya
tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali
huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza
alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Wakati Mapinduzi hayo yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa nchini Tanzania kujumuika na
viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa
Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Baada
ya tangazo la kupindulikwa kwake, Rais huyo alipanda ndege
kurejea nchini kwake licha ya tangazo la kufungwa kwa mipaka
yote na viwanja vya ndege.
Kwa
mujibu wa taarifa ya BBC asubuhi hii ya mei 14, Ndege ya
Rais huyo haikuweza kutua nchini Burundi na badala yake
ilirudi tena Tanzania ambapo mpaka sasa Rais Nkurunzinza yupo
jijini Dar es Salaam- Tanzania
No comments:
Post a Comment