Rais Kikwete Kufungua Mkutano wa Mpango wa Uendeshaji - LEKULE

Breaking

20 May 2015

Rais Kikwete Kufungua Mkutano wa Mpango wa Uendeshaji

 RAIS Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi (OGP).

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21, mwaka huu katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Dhumuni la  mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.

“Kupata uzoefu wa utekelezaji wa OGP kutoka nchi wanachama katika bara la Afrika nan je ya Afrika kama vile taarifa za uwazi zinazoimarisha uwajibikaji” ilieleza taarifa hiyo.

Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika nchini na wa pili kwa Kanda ya Afrika ambapo kwa mara ya kwanza  ulifanyika nchini Mombasa nchini Kenya mwaka 2013.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki 200 kutoka Serikalini, Asasi za kirai, Washirika wa Maendeleo wakiwemo Mawaziri kutoka ndani na nje ya nchi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali, wawakilishi kutoka Nchi wanachana wa OGP kutoka bara la Afrika.

Washiriki wengine ni kutoka nchi za Botswana, Zambia, Uganda, Marekani, Zimbabwe pamoja na washirika wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia, UNDP, UNICEF, UNESCO, MCC, USAID, DFID na JICA.

No comments: