Dodoma. Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amemtaja mrithi wake baada
ya kuwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kumchagua mgombea urais
anayekubalika ndani na nje ya chama hicho.
Kikwete
alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha Halmashauri Kuu kwenye
ukumbi wa ofisi ya makao makuu ya chama hicho mjini hapa, unaojulikana
kwa jina la White House.
Kauli hiyo imekuja wakati
chama hicho kikiwa kwenye wakati mgumu kupata mgombea mpya baada ya Rais
Kikwete kumaliza muda wake wa vipindi viwili vinavyokubalika kikatiba,
huku kukiwa na ongezeko kubwa la nguvu ya upinzani.
Juzi,
Kamati Kuu ya CCM iliwaachia huru makada wake sita waliotumikia adhabu
ya miezi 17 ya kuzuiwa kujishughulisha na shughuli za uchaguzi baada ya
kubainika kukiuka sheria za uchaguzi za chama hicho kutokana na kuanza
kampeni mapema.
Miongoni mwa makada hao, wamo wanaopewa
nafasi kubwa ya kupitishwa na chama hicho na ambao kambi zao zimekuwa
zikipambana vikali na kuweka wasiwasi wa kuivuruga CCM.
Lakini
Kikwete, ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, alionekana kufahamu hali
inayoendelea na alitumia muda huo kueleza jinsi ambavyo CCM imejidhatiti
kupata mgombea urais kwa kuzingatia maslahi ya chama hicho na ya
Watanzania, akisema wakati wa kudhani mtu yeyote anayeteuliwa na chama
hicho atachaguliwa na wananchi umeshapita.
Akizungumza
kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Rais Kikwete alisema kikao cha
Halmashauri Kuu kina umuhimu wake kwa sababu kitaamua ushiriki wa CCM
katika Uchaguzi Mkuu na kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea wa chama
hicho.
Rais Kikwete alisema watu wote wanachama na wasio wanacham wanasubiri kwa hamu uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.
“Watanzania
wote bila kujali itikadi zao wanaitazamia na kuitumainia CCM kutoa
uongozi ulio bora kwa nchi yetu. Hali hii inathibitisha uleusemi wa Baba
wa Taifa kwamba Rais anaweza kutoka chama chochotelakini rais bora
atatoka CCM,” alisema.
Alisema CCM inatakiwa kutambua
na kuzingatia uzito wa wosia huo wBaba wa Taifa na kuhakikisha kuwa
unatekelezwa kwa ukamilifu wake.
“Asiyesikia la mkuu
huvunjika guu. Vikao vya Kamati Kuu, HalmashauriKuu ya Taifa na Mkutano
Mkuu wa Taifa, vina jukumu maalumu la kuongozna kusimamia mchakato wa
uteuzi ndani ya chama, utakaotuwezeshkupata wagombea wanaofaa,”alisema.
“Wenye
kukidhi kiu na matarajio ya wanachama wa CCM na wananchi waJamuhuri ya
Muungano wa Tanzania ni sisi. Lazima tupate wagombewanaochagulika,
tunapowapeleka kwa wananchi ambao wengi wao siywanaCCM.”
Alisema CCM wako milioni sita lakini wapigakura ni milioni 23, kwa hiyo lazima wapate mtu ambaye wananchi watamkubali.
Rais
Kikwete alisema wakimpata mtu ambaye wao CCM inampenda, lakinwananchi
hawatampenda, chama hicho kitaumia.“Lazima tupate wagombea ambao
wananchi watasema ‘naam’, tusipatwagombea ambao watu wataguna. Watasema
‘eeh yaani CCM wamemleta huyu? Tutauweka ushindi kwa CCM rehani. Ndugu
zangu lazima tutambue kuwa wakati umebadilika,”alisema.
“Ni
ngumu sana kwenye chama chetu ukiwaambia kuwa wakati umebadilika na
tunaweza kushindwa, wanakuwa wagumu sana, lakini mnajidanganya tu,
lazima tujue kwamba wakati umebadilika... ile dhana kuwa yeyotatakayeteuliwa na CCM atashinda imeshapitwa na wakati.”
Rais Kikwete alisema dhana ya kuwa wakichagua mtu yoyete mradi katokCCM, watakuja kukiona cha mtema kuni.
“Hivyo
ni lazima tupate wagombea wanaochagulika na wananchi ambao niwengi
kuliko wanaCCM. Hatuwezi kupeleka kwa wananchi watwasiokubalika, watu
waliopungukiwa sifa, tukadhani Watanzania watamchagua tu kwa sababu ni
mgombea wa CCM,”alisema.
“Lazima tuwe na wagombea
watakaopendeza kwetu na watakaopendeza kwWatanzania. Wagombea ambao watu
wataamini kuwa wako salama, nchi,jimbo, kata zipo katika mikono
isiyokuwa na shaka.”
Alisema wakipeleka wagombea wanaowapendeza wao bila kuwapendeza wananchi, watakula hasara.
“Tutajipa
kazi kubwa ya kufanya na kuna hatari ya kushindwa. Lazima tusome alama
za nyakati. Tutambue zaidi watu wanachukizwa na watu wa namna gani?
Tusipeleke mtu anayeakisi mambo yanayochukiza watu na kujiaminisha kwa
historia na nguvu ya Chama cha Mapinduzi atashinda hampiti nimesema
wakati ule ndugu zangu umekwisha,”alisema.
“Tusidanganyane
kwamba sisi tunapendana au tunaogopana, wananchi hawatatuogopa.
Wananchi hawatakuogopa wala hawatasita kuonyesha kwamba hawapendezwi
naye. Tukifanya uteuzi mbaya wa wabeba bendera kwa urais, wabunge
wawakishi madiwani hasira za wananchi zinaweza kuwa kwa chama kizima na
kuadhibu wagombea wetu ngazi nyingine.”
Alisema wakipata mgombea ambaye wananchi wataguna, wananchi wanaweza wakapata hasira na wakawakataa wagombea wote.
Rais
Kikwete alitoa mfano wa chama cha nchini Canada ambacho kilikuw
kikiongoza tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia, lakini kilipoenda katika
uchaguzi kikashindwa hata kuwa chama kinachoongoza katika upinzani ndani
ya Bunge.
“Ndiyo maana nasema sisi tusilewe historia kwamba chama kikubwa.
Tukifanya makosa hatutafika. Tusikubali kukifikisha chama chetu hapo kwa sababu ya urafiki. Chama kwanza, mtu baadaye,” alisema.
Alisema
bahati nzuri CCM ina misingi mizuri ya kupata wagombea wake,labda
waamue wenyewe kutoiheshimu misingi hiyo ambayo imejengwa katikkanuni na
taratibu za kuwapata wagombea.
Rais Kikwete alisema
CCM ina maadili na miiko yake ya kuzingatia taratibu na kwamba miiko
hiyo imejaribiwa na kutumika na kuwapata wagombea wazuri waliokiletea
chama ushindi na heshima katika chaguzi zilizopita.
“Nawaahidi
hatutayumba wala hatutaogopa katika kusimamia misingi hii mizuri ya
chama chetu, kwa nia ya kukumbushana dhima na wajibu wwanachama na
viongozi tulio nao katika kulitekeleza hili,” alisema.
Aliwataka kuongozwa na kuweka masilahi mapana ya chama chao, kulikmasilahi ya mtu mmoja mmoja.
“Nayasema
haya kwa sababu naona kumekuwepo kujisahau au kujifanya kuwa umesahau
miongoni mwa wagombea wa uteuzi na hata miongoni mwa wajumbe wa
Halmashauri Kuu na viongozi wengine wa chama na hatwanachama kwa kufanya
mambo mengine yaliyo kinyume na misingi ychama,” alisema.
“Tusitoe
nafasi ya kukimong’onyoa chama, haiwezekani yanaposema aminaposikika
minong’ono baina ya wagombea, washabiki na baadhi yettukiwemo humu
(Nec), hayanifurahishi hata kidogo.”
Alisema watu kufanya mambo yaliyo kinyume na uteuzi ndani ya chamamambo yasiyokubalika, hayataachwa yapite.
“Naomba
myazingatie ili mrahisishe kazi ya uteuzi, tujadili tu historia ya mtu
na uwezo wake kwa nafasi anayoiomba. Isiwe tunapoteza muda mwingi
kujadili makando kando, mambo yanayofanyika kinyume cha utaratibu.
Utafanyaje mambo kinyume cha utaratibu unataka kukipeleka wapi chama
chetu?
“Mnataka iweje, tuseme hakuna kilichofanyika? Haiwezekani hatuwezi
kunyamaza
tutakuwa tumepoteza dhamana yetu. Tunao wajibu wa kusimamia misingi
tuliojiwekea na kikao hiki ndicho chenye dhamana hiyo,alisema.
Alisema
wamedhamiria kusimamia bila ajizi, bila kupendelea na kwamb wana wajibu
wa kutenda haki na watafanya hivyo na bila shinikizkutoka kwa mtu
yoyote.
“Bila shaka viongozi wenzangu tumeelewana, tusaidiane ili tuvuke vyema,” alisema.
Alisema Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 bado inaandaliwa na imefikia
mahali pazuri na kwamba kikao kijacho itapelekwa.
Katika hatua nyingine, Kamati Kuu ya CCM imeishauri Serikali kukutana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nec, kutafakari namna bora ya kushughulikia kura ya maoni kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa CCM imeangalia changamoto zilizopo na hivyo kutoa ushauri huo.
“Moja ya changamoto ni suala la uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Wapigakura,” alisema.
Kamati Kuu jana mchana ilimaliza kikao chake kilichofanyika kwa siku mbili.
Kamati hiyo ilikutana tangu juzi saa 10:00 jioni na kuendelea hadi saa nane za usiku wa kuamkia jana.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa kamati hiyo ilikuwa bado haijamaliza baadhi ya ajenda na hivyo kukutana tena jana saa sita mchana hadi walipomaliza alasiri na ndipo Halmashauri Kuu ya Taifa ilianza kikao chake saa 10 alasiri badala ya saa nne asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya CC, zilidai kulikuwa na mvutano kuhusu ratiba ya mchakato wa kutafuta wagombea wa nafasi za urais, ubunge, udiwani na uwakilishi kutokana na muda kuonekana kuwatupa mkono na kanuni.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya CC, kilidai kuwa suala la ratiba lilikuwa na mvutano kwakuwa muda umekwenda.
Kwa mujibu wa utaratibu, wanaoomba nafasi ya kuteuliwa kugombea urais, lazima wapate muda wa kutafuta wadhamini katika mikoa mbalimbali ya Bara na Visiwani.
Wagombea hao baada ya kupata wadhamini wanatakiwa kupita kwenye mchujo wa vikao vya chama, kuanzia Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na baadaye Mkutano Mkuu.
Baada ya kupatikana mgombea urais, jina lake linatakiwa kupelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nec, ambako nako hutolewa muda kwa wanaotaka kuweka pingamizi.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa CC pia ilikuwa na changamoto kuhusu kanuni, na kuna taarifa baadhi ya wabunge wanataka kanuni kanuni zimtambue mbunge kuwa ni mjumbe halali wa Halmashauri Kuu.
Hali ilivyokuwa
Jana asubuhi kabla ya kikao cha CC, kilianza kikao cha Kamati Maalumu ya Zanzibar ambao walikuwa wakipitisha majina ya wagombea katika nafasi za uongozi wa chama kupitia Shirikisho la Vyuo Vikuu.
Wajumbe wajumbe wa Nec waliambiwa kikao kingeanza saa nne, lakini baadaye zikasambaa taarifa kwamba CC ilikuwa haijamaliza baadhi ya ajenda, wajumbe wakalazimika kuendelea kusubiri, lakini baadaye walipewa makablasha kwa ajili ya kujiandaa na kikao chao kilichoanza saa 11 jioni.
Hata hivyo, mmoja wa wanaotafuta kuteuliwa kuwa wagombea urais alionekana akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Nec akiwathibitishia yuko ‘serous’.
Mmoja wa wajumbe wa Nec alithibisha kwamba alifuatwa na mgombea huyo akiomba aungwe mkono.
Pia baadhi ya mashabiki wa watangaza nia walikuwepo wakiwa kwenye makundi yaliyoashiria ni kupanga mikakati ya kukubalika.
Noti zamwagwa
Taarifa zingine zilidai kuwa juzi watangaza nia wawili walio kwenye nafasi za uwaziri, walianza kumwaga fedha wa wajumbe wa Nec, mmoja anaelezwa kutoa ‘mshiko’ wa Sh300,000 kwa kila mjumbe na mwingine alimwaga ‘mshiko’ wa Sh500,000 kwa wajumbe.
Baadhi ya wajumbe ambao hawakupata ‘mshiko’ huo waliliambia gazeti kwamba, wamesikia wenzao wamepewa lakini wao hawakupewa.
Baa zafurika
Baada ya taarifa za kufutwa kwa kifungo kwa makada sita, waliofungiwa kwa kukiuka kanuni za kuanza kampeni mapema, baa nyingi katika mji wa Dodoma, zilifurika baadhi ya wapambe wa watangaza nia, ambapo walikunywa na kula wakishangilia uamuzi wa CC wa kuwafungulia makada hao.
Hata hivyo, hali hiyo ilikuwa tofauti na upande wa watangaza nia waliotaka mmoja wao akatwe, ambapo wa wapambe hao ambaye ni mbunge (jina linahifadhiwa) alisikika akimweleza mwenzake kuwa “mjomba tumekufa”.
Zanzibar watoa neno
Vyama vya Upinzani Zanzibar vimepongeza hatua ya CC ya kuwaachia huru makada wake sita ambao walifungiwa kushiriki harakati za kisiasa baada ya kwenda kinyume na maadili ya kuanza kampeni mapema kabla ya utaratibu wa chama kutangazwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Viongozi wa TADEA, CHADEMA, CUF, CCM, ADC walisema kitendo cha CCM kuwachukulia hatua makada wake sita, ambao ni viongozi mashuhuri ni mfano tosha kuwa chama hicho hakijali mkubwa wala tajiri katika kusimamia miiko na maadili ya chama.
“Sisi kama TADEA tunawapongeza CCM kwa kusimamia taratibu na misingi ya demokrasia na hii ni fundisho kwa vyama vyengine kuheshimu miiko na maadili ya chama” alisema Juma Ali Khatib, Katibu Mkuu wa Tadea.
Hata hivyo, alisema kwamba katika kipindi kama hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi pilikapilika pamoja na harakati za nje ya mfumo wa chama haziwezi kukwepeka kwa sababu hakuna wapambe wanaoweza kukaa kimya bila ya kumfanyia kampeni mgombea wao.
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa ADC, Ali Makame Issa alisema kwamba kuna mambo ya kujifundisha kutoka CCM kama chama ambacho hakijali cheo cha mtu, sifa au uwezo wake, na kusimamia maadili kwa vitendo tofauti na vyama vyengine.
Alisema CCM kama chama tawala lazima kiangalie kitarudisha vipi umoja baada ya kupata jina moja la mgombea wake wa nafasi ya Urais, na kusisitiza upo umuhimu wa kuzingatia haki na usawa na kuondoa mizengwe katika kupata jina la mgombea wa chama hicho.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chadema Mkoa wa Mjini Magharibi (BAVICHA) Francis Werema alisema CCM imejitisha yenyewe ndio maana imeamua kuwafungulia makada wake baada ya kuona hawana mtu mwenye sifa ya kuwania Urais zaidi ya watu sita waliokuwa wamefungiwa.
“Wamehofia kuathiri uhai na umoja wa chama chao katika kuelekea uchaguzi mkuu, baada ya kuona wamejitokeza wagombea wengi , wengine wakikosa sifa za kushika nafasi hiyo ikilinganishwa na makada sita waliofungiwa” alisema Werema.
Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe alisema uamuzi wa kuwafungulia makada sita ni mbinu ya kuwaziba macho watu, kwa vile huwezi kumfungia mtu kwa makosa yaliyothibitika na baadae kupata msamaha.
Alisema kwamba chama chochote kinahitaji kusimamia kwa vitendo harakati na shughuli zake za kisiasa kwa kuzingatia miiko na maadili na ndio maana CUF imeagiza kitengo cha ulinzi cha chama hicho kuanza kufuatilia na kuchunguza wabunge na wawakilishi ambao wanatuhumiwa kutumia ushawishi wa rushwa wakati wa zoezi la kura za maoni.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Mjini, Baraka Shamte alisema kwamba adhabu iliyokuwa imetolewa na chama imeweka msingi wa nidhamu kwa viongozi lakini alisema wakati umefika miiko na maadili ya chama yasimamiwe kuanzia ngazi ya tawi, wilaya hadi mkoa, kwa sababu kuna viongozi wanaokiuka miiko na maadili ikiwemo Zanzibar.
“Hata majambazi wana maadili yao, wanalishana hadi yamini yakutokutoa siri, na wapo tayari kufa napongeza sana hatua iliyochukuliwa ya kuwasamehe,” alisema Baraka Shamte.
Shangwe za wanachama wa CCM zilianza kujitokeza katika maskani mbalimbali zanzibar, muda mfupi baada ya kutolewa kwa taarifa za kusamehewa kwa makada sita waliokuwa wamefungiwa kujulikana huku Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa akipewa nafasi kubwa katika mazungumzoa ya wana maskani ikiwemo maskani Kaka ya Kisonge, Naushad Maskani Jang’ombe, Dk.Omar maskani, pamoja na baraza mbalimbali za wanachama wa kambi ya upinzani pia walionekana kufuatilia taarifa hizo kupitia vituo vya radio na televisheni zanzibar.

No comments:
Post a Comment