Dar/Mashirika. Rais wa Burundi, Pierre
Nkurunziza amewasili jijini Bujumbura ikiwa ni siku mbili baada ya waasi
kutangaza kumuondoa madarakani na tayari majenerali watatu waliotangaza
mapinduzi wamekamatwa huku wanajeshi 12 wakiuawa.
Awali,
kulikuwa na taarifa kuwa kiongozi wa uasi huo, Meja Jenerali Godefroid
Niyombare alikuwa amekamatwa pamoja na wasaidizi wake, lakini baadaye
mshauri wa habari wa rais, Willy Nyamwite alisema alipewa taarifa zisizo
sahihi.
Lakini wakati kukiwa na habari kuwa Meja
Jenerali Niyombire amekamatwa, waasi hao wamesema wataendeleza vita
dhidi ya majeshi ya Serikali kwa ajili ya kumuondoa Rais huyo ambaye
anapingwa kutokana na kutangaza kugombea urais kwa mara ya tatu kinyume
na katiba.
“Amekamatwa, alikataa kujisalimisha,”
Gervais Abayeho, msemaji wa Rais Nkuruzinza aliliambia Shirika la Habari
la Uingereza, Reuters.
Msafara wa Rais Nkurunziza
ulionyeshwa kwenye televisheni ukiwasili jijini Bujumbura, ingawa picha
hizo hazikumuonyesha Rais huyo ambaye alipitia kijijini kwake Ngozi
kabla ya kwenda jijini humo akitokea Tanzania.
Mnadhimu
wa Jeshi, Jenerali Prime Niyongabo, akizungumza kwa mara ya kwanza
tangu majeshi yanayomtii Nkurunziza yadhibiti redio na televisheni ya
serikali, alisema wanajeshi 12 wa upinzani waliuawa wakati wa mapambano
ya kuwania kituo hicho juzi.
Alisema wanajeshi wengine 35 wa uasi walijeruhiwa na 40 wamejisalimisha.
Alisema wanajeshi wanne wa Nkurunziza walijeruhiwa.
Hali
ya jijini Bujumbura ilikuwa shwari jana baada ya mapambano kutawala
siku nzima ya juzi wakati majeshi yanayomtii Nkurunziza yalipokuwa
yakipambana kukomboa sehemu muhimu.
“Tunatoa wito kwa
wakazi wa Manispaa ya Bujumbura kufungua tena biashara zao. Hali sasa
imesharejea kuwa ya kawaida baada ya kushindwa kwa waasi,” Meya wa
Bujumbura, Saidi Juma aliliambia shirika la habari la China, Xinhua.
Baada
ya kuwasili, Rais Nkurunziza alipewa taarifa fupi ya mapinduzi na hata
jinsi jeshi lilivyofanikiwa kuzima uasi na kutwaa tena miji ya
Bujumbura.
“Rais Pierre Nkurunziza sasa yuko Burundi,” Msemaji wa Serikali, Willy Nyamitwe alisema.
“Hicho ndicho tunachoweza kusema kwa sasa.”
Jenerali
Cyrille Ndayirukiye, msaidizi wa kiongozi wa mapinduzi hayo, alikiri
kuwa jitihada za kuuangusha utawala wa Nkurunziza zimeshindikana.
“Binafsi, nakiri kusema, mipango yetu imekwama,” alisema Jenerali Ndayirukiye.
“Tulipambana tukijua kuwa tutaungwa mkono na jeshi.”
Wakati mapinduzi hayo yakifanyika, Nkurunziza alikuwa Tanzania kwa ajili ya mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi ulioibuka baada ya kiongozi huyo kutangaza kuwa atagombea urais kwa kipindi kingine cha tatu, kitu ambacho wapinzani wake wanasema ni kinyume cha katiba.
Mkurugenzi wa kituo kimoja cha redio, Jerome Nzokirantevye alisema askari wanaomtii Nkurunziza wameshadhibiti sehemu zote muhimu za Bujumbura, ikiwa ni pamoja na kituo cha redio na televisheni ya Serikali na Uwanja wa Ndege wa Bujumbura.
Tangu kuanza kwa machafuko hayo, zaidi ya Warundi 100,000 wamekimbilia Tanzania, Rwanda na Uganda.
‘Wanamapinduzi’ wakamatwa
Majenerali wa kijeshi walioendesha jaribio la mapinduzi, tayari wametiwa mbaroni ikiwa ni saa chache baada ya Rais Nkurunziza kurejea nyumbani akitumia njia ‘zisizofahamika’.
Hata hivyo, ripoti zilisema kuwa kiongozi wa mapinduzi hayo, Jenerali Godefroid Niyombare alitoroka muda mfupi baada ya kuzingirwa na vikosi vya askari wanaomtii Rais Nkurunziza.
Inasadikika kuwa jenerali huyo amejificha kusini mwa mji wa Bujumbura na kwamba wapiganaji wake wanaendelea kushikiliwa.
Maofisa wa jeshi walisema kuwa bado wanaendelea kumsaka jenerali huyo ambaye awali alikiri kuzidiwa nguvu kiasi cha kuonyesha wasiwasi kuhusu usalama wa maisha yake.
Akizungumza na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP mapema jana, Jenerali Niyombare alisema kuwa jaribio la kuiondoa serikali iliyoko madarakani limeshindwa na wapiganaji wake walianza kujisalimisha.’
Naye msemaji wa waendesha mapinduzi hayo, Venon Ndabaneze alikiria pia kushindwa kwa jaribio lao akisema kuwa baadhi ya wapiganaji wao walikamatwa na vikosi vya serikali. Miongoni mwa waasi wanaoshikiliwa ni pamoja na msaidizi wa kiongozi wa mapinduzi hayo, Cyrille Ndayirukiye.
Marekani yawaonya raia wake
Marekani imewaonya raia wake kwenda nchini Burundi na kuwataka wale walioko ndani kuondoka haraka iwezekanavyo. Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kuwa Burundi inakabiliwa na hali mbaya ya usalama, hivyo ni muhimu kwa raia hao kuchukua tahadhari mapema.
Taarifa hiyo iliwataka raia wote wa Marekani kutotembea ovyo na hata wale wanaotaka kuondoka kuangalia maeneo ambayo ni salama,” inasema taarifa hiyo.
Hata hivyo, mitaa mbalimbali ya jiji la Bujumbura ilikuwa imetulia na zaidi walikuwa wakionekana askari wanaomtii Rais Nkurunziza wakiwa katika vizuizi, ikiwemo Barabara Kuu ya Kusini mwa Bujumbura.
Uchaguzi Mkuu palepale
Utawala wa Rais Nkurunziza umesisitiza kuendelea na shughuli za Uchaguzi Mkuu ukisema kuwa utafanyika kama ulivyopangwa.

No comments:
Post a Comment