Kikao kikiwa kinaendelea jana usiku.
Mwenyekiti wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Bw. Mugwengezo Chauvineau akiongea na waandishi wa habari Serena Hotel Dar jana usiku .
Dkt. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa nchini Burundi, akiongea na waandishi wa habari jana usiku.
Mwenyekiti wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi kwa mara ya kwanza amefika nchini Tanzania ili kuweza kushuhudia mkutano wa dharula kati ya viongozi watano wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu nchi ya Burundi ambayo sasa imeingia katika machafuko baada ya Rais aliyepo madarakani kutaka kuongeza muda wake.
Akiongea na waandishi wa habari usiku kuamkia leo, Mkuu huyo wa vuguvugu la maandamano ya Burundi amesema kuwa wananchi hawaridhiki na Rais wao kuendelea kuwa madarakani ambapo hata sheria na katiba hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu ambapo wananchi wanaendelea kupinga Rais kuendelea kuwania kwa muhura wa tatu.
Amezungumzia juu ya waandamanaji baada ya wiki tatu bado wapo barabarani ambapo wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa sababu wanadai kumekuwa na mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru waandamanaji hao kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kuwa wameweza kudhihilisha na kuwa walikuwa ni watulivu na kutulia kungoja utekelezaji wa mambo ambayo yamezungumziwa.
Amesema kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi ya laki mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate kurejea nchini kwao.
Pia ameiomba Jumuia ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea kwa sasa Nchini Burundi ambapo jumuia iyo tangia zamani imeweza kusimamia mambo ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi iweze kufikia malengo ya Mkataba wa amani wa Arusha na kufikia malengo ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.
Kuhusu jaribio la mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo miongoni mwa wale ambao wameandaa tukio hilo
Kuhusu jambo baya alilofanya Rais wa Burundi, kiongozi huyo amaesema kwamba ni kuongezea muhula wakati tayari alisha tawala kwa miaka 10, na katika miaka hiyo alishindwa kuweka usawa baina ya warundi, hajatekereza swala la haki za Binadamu , aliongeza kuwa muhula wake ni muhura baki na haramu hauko sambamba na Katiba wala Sheria ya Burundi pamoja na Mkataba wa Arusha na angetekeleza yote hayo hizi vurugu zisinge kuwepo.
Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu. Pia Warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena damu inamwagika.
Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama mkutano na kuhakikisha maamuzi yote yanafanyiwa kazi.
Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya tatu.

No comments:
Post a Comment