Mrema Akanusha Kufukuzwa TLP - LEKULE

Breaking

22 May 2015

Mrema Akanusha Kufukuzwa TLP

MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustino Mrema ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Vunjo amekanusha kufukuzwa katika chama chake.
 


Alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya kuzagaa habari kuwa yeye sio Mwenyekiti wa chama hicho.
 


Alisema amekuwa akishangazwa na habari zinazotolewa na kikundi cha watu wanaojiita wanakamati wa TLP ambao wanadai kuwa yeye sio Mwenyekiti kwani tayari wamemchagua mwenyekiti wao.
 


Aliongeza kuwa kama kuna mabadiliko katika chama hicho, ni lazima yeye ajue kwani ndiye pekee mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko katika chama hicho.
 


“Mikutano yote lazima iitishwe na mimi, hakuna mwenye mamlaka kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, hivyo hakuna mtu mwenye ubavu wa kunivua uenyekiti,” alisema Mrema.

No comments: