MOI Yaongoza kwa Upasuaji Kidunia - LEKULE

Breaking

30 May 2015

MOI Yaongoza kwa Upasuaji Kidunia

TAASISI ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imetangazwa kitovu cha weledi duniani katika upasuaji wa mfupa mrefu wa paja na wa chini ya goti kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wenye mafanikio makubwa kuliko nchi nyingine yeyote duniani.
 
Akizungumza na Mpekuzi  jana jijini Dar es Salaam Meneja Ustawi na Uhusiano wa Taasisi hiyo Almas Jumaa, alisema zaidi ya Zaidi ya wagonjwa 4800 wamefanyiwa  upasuaji wa mifupa mirefu toka Mwaka 2008.
 
Alisema katika mwaka huo Taasisi ya MOI ilianza kutumia utaalamu wa kutibu mifupa iliyovunjika kwa kuweka vyuma maalum vinavyojulikana kama ‘SIGN NAIL’ tiba ambayo inamfanya mgonjwa aweze kupona kwa haraka na aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
 
Alisema kutokana na mafanikio hayo ya kutibu wagonjwa wengi na kwa weledi nchi nyingine duniani zimekuwa zikija kwenye taasisi hiyo kujifunza.
 
“Juzi tulimaliza mafunzo ya siku tatu ambayo yalikutanisha wataalamu wa upasuaji kutoka nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kujifunza namna ya kutibu mifupa mirefu na mingine kama kiunoni na chini ya goti kwa kutumia teknolojia ya kuweka vyuma,” Alisema Jumaa.
 
Allizitaja nchi zilizohudhuria mafunzo hayo kuwa ni pamoja na Nigeria, Zimbabwe, Ethiopia, South Sudan, Liberia, Haiti na Marekani.
 
Alibainisha kuwa, madaktari bingwa kutoka Marekani waliwafundisha mbinu   ya kufidia kipande cha mfupa kilichopotea baada ya ajali kwa kuweka mfupa wa bandia na kuunganisha mfupa hivyo kumuondoa mgonjwa katika hatari ya kupoteza kiungo kurudi katika hali ya kawaida.

No comments: