Miswada 9 ya Sheria Yasainiwa na Rais Kikwete - LEKULE

Breaking

15 May 2015

Miswada 9 ya Sheria Yasainiwa na Rais Kikwete

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Kikwete ameshasaini miswada 9 katika ya 14 iliyopitishwa na bunge katika mkutano wake wa 19 ukiwemo wa sheria ya makosa ya mitandao pamoja na muswada wa sheria ya takwimu iliyozua utata.
 
Akitoa taarifa kuhusu kusainiwa kwa miswada hiyo leo Bungeni Spika wa Bunge Anna Makinda amesema miswada mitano iliyobaki atatolea ufafanuzi baada ya kupata kibali kutoka kwa Rais.
 
Makinda ametaja Miswada mingine iliyosainiwa ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani, Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha, Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kiektoniki pamoja na Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa.

No comments: