KANISA
la Moravian Jimbo la Mashariki limeitaka Serikali iangalie upya uamuzi
wake wa kuruhusu mgawanyiko wa kanisa hilo kwa kuruhusu usajili wa Jimbo
lingine ili kuepusha uvunjifu wa amani.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jimbo la
Mashariki,Dkt Clement Fumbo ambapo alisema endapo serikali itaruhusu
hilo basi iruhusu na upande wao kusajili na kuendesha masuala yake ili
kuwa na amani.
“Tunaiomba
serikali iwatahadharishe upande uliosajili Jimbo wasijihusishe na
makanisa au shirika ambazo haziko upande wao kwa kutumia usajili
walioupata vinginevyo watachukuliwa wamekwenda kuleta fujo”alisema Fumbo.
Aidha
aliitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo inajua mgogoro uliopo kati ya
pande mbili tangu zamani kuwasiliana na pande zote ili kujua
kinachoendelea kabla ya kusajili Jimbo jipya.
Clement
alisema kuwa ni kwa muda mrefu Kanisa la Moravian jimbo la misheni ya
Mashariki limekua na mgogoro ambao umeigusa jamii kutokana na machafuko
ndani ya nyumba za ibada.
“Mgogoro
huo umefikia mahali pa kuligawa kanisa hili katika makundi mawili huku
kila kundi likiwa na Halmashauri yake iliopelekea kutokea kwa machafuko
katika mashirika mbalimbali ikiwemo ushirika wa Kinondoni”alisema Fumbo.
Alisema
tamko hilo ni kutokana na taarifa za kusajiliwa kwa jimbo la upande wa
pili huku ikisemekana uzinduzi wa Jimbo hilo jipya ukitegemewa
kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mgogoro
huo ulipelekea kanisa la Moravian Duniani lenye Makao Makuu nchini
Norway kuingilia kati na kutaka kuondoa kesi inayowafanya walumbane
mahakamani.
Hali
hiyo ilitokea baada ya kuondolewa nyadhifa na kusimamishwa kazi,
Mwenyekiti wa Halmashauri Jimbo hilo, Clementi Fumbo na wenzake saba.
Fumbo
na wenzake saba walifungua kesi ya madai namba 222 ya mwaka 2012,
katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam wakipinga
kuondolewa madaraka na kusimamishwa kazi.
No comments:
Post a Comment