MSTAHIKI Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amesema hana sababu ya kuendelea kujibizana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema), kwani amekuwa akimpa changamoto za kiutendaji ambazo zimemfanya kufanya kazi kwa ufanisi.
Amesema, mbunge huyo anaapswa kusubiri kubali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili aweze kutumia vema jukwaa la kisiasa kuliko ilivyo sasa anavyotumia Bunge kuwachafua watu wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Mbeya, Meya Kapunga, alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kuhusu hali halisi ya utendaji kazi wake uliokuwa umezungukwa na majungu, chuki na fitina zisizokuwa na msingi zinazoendelea kutolewa na Mbunge ‘Sugu’ ambaye alimfananisha sawa na chipukizi wa kisiasa.
“Leo (jana), asubuhi nimemsikia Sugu, akizungumza bungeni kuhusu ugawaji wa Jimbo la Mbeya Mjini na kunitaja mimi ni miongoni mwa viongozi wanaoshinikiza kugawanywa kwa jimbo hili, wala sikatai ni kweli kwani mchakato huu wa kuligawa jimbo hili niwa muda mrefu kabla ya Sugu kuingia ulingoni,” alisema Kapunga
Alisema, mchakato wa kuligawa jimbo hilo, ulianza mwaka 2008 ukiwa chini ya Mbunge Mpesya hivyo yeye kama Meya ni jukumu lake kulisemea hilo kama mtendaji wa halmashauri.
“Hapa kosa langu nini mpaka Sugu kunisema bungeni, kwanza nimeona ni mtoto anayezoea tabia mbaya, kukaa kila saa ananisema bungeni anaonyesha ni jinsi gani asivyokomaa kisiasa,” alisema
Alisema, Sugu ni mjumbe wa vikao vya kiutendaji vya halmashauri ana nafasi kubwa ya kufika na kuyazungumzia hayo tatizo linalomsumbua ni upeo wake mdogo wa kufikiri hivyo kujiaminisha kwambajimbo la Mbeya ni mali yake.
Alisema, Mbeya ni mali ya wananchi, si la ukoo na kitendo cha kuwaza jimbo ni mali yake ni ujinga, yeye atabaki kuwa kwenye orodha ya wabunge wa ajaabu ambao kila siku kazi yake ni kumuwaza Kapunga badala ya kusimama na hoja.
“Mimi ninamsubili huku kwa wananchi, sasa ngoja nimuache tu aendelee na utoto na jambo la kumsikitikia ni kwamba mpaka leo anaamini akili za wanambea wa miaka mitano iliyopita ziko palepale,” alisema
No comments:
Post a Comment