Bungeni: Serikali yamkalia kooni Mwanamuziki Shilole kwa Picha zake za Uchi - LEKULE

Breaking

29 May 2015

Bungeni: Serikali yamkalia kooni Mwanamuziki Shilole kwa Picha zake za Uchi



Sakata la Mwanamuziki Shilole kucheza huku baadhi ya sehemu za matiti zikiwa wazi limechukua sura mpya Bungeni leo kufuatia Naibu Waziri wa Habari vijana na Utamaduni na Michezo Juma Nkamia kutangaza kuwa inasubiria uamuzi wa Baraza la sanaa Taifa (Basata).

Aidha, Nkamia amesema suala la shilole hivisasa lipo chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo mara baada ya kumaliza mahojiano naye litapelekwa wizara ya habari vijana na utamaduni na michezo kwa hatua nyingine zaidi.

Hivi karibuni Shilole aliwaomba msamaha watanzania kwa madai kuwa anajutia kutozingatia maadili katika onesho hilo lililofanyika nchini Ubelgiji na kuzua gumzo nchini Tanzania.

No comments: