Dar/Mashirika. Jeshi la Ulinzi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), limesema majina ya wapiganaji wa Tanzania waliofariki
dunia kwa kushambuliwa na waasi wa ADF huko Jamhuri ya Demokrasia ya
Congo (DRC) yatatajwa baada ya miili hiyo kuwasili nchini.
Msemaji
wa JWTZ, Meja Joseph Masanja alisema jana kuwa kwa sasa wanasubiri
maelekezo na taratibu za kuleta miili hiyo zikamilike.
Masanja
aliwatoa hofu Watanzania kuhusu usalama wa askari wake walioko DRC,
wanaoshiriki operesheni ya kulinda amani chini ya vikosi maalumu vya
Umoja wa Mataifa.
Meja Masanja alisema kikundi cha
wanajeshi 46 ambao ni walinzi wa amani kilisafiri kwa helikopta kutoka
Mji wa Abialose kuelekea Mavivi na baada ya kufika walikwenda Mayimoya
kwa gari. “Wakiwa njiani walishambuliwa na ADF kwa silaha za kivita na
gari moja kuteketezwa na kusababisha vifo vya askari wetu na wengine 16
kujeruhiwa,” alisema.
Tukio hilo linafanya idadi ya
wanajeshi wa Tanzania waliouawa nchini humo kufikia watatu baada ya
askari mwingine, Khatibu Mshindo kuuawa Agosti 2013 katika shambulio la
bomu lililofanywa na waasi wa kikundi cha M23 kwenye Mji wa Goma ulioko
Mashariki mwa DRC.
Msemaji wa Mpango wa Kulinda Amani
kutoka Umoja wa Mataifa, DRC, Felix Basse alikaririwa na Shirika la
Habari la AFP akisema mashambulizi ya juzi yalifanyika katika Kijiji cha
Kikiki kilichoko kilomita 37, Kaskazini-Mashariki mwa mji wa Kivu.
Habari nyingine zilizopatikana jana, zilisema kuwa askari wa Tanzania wameingia msituni kusaka waasi wa Uganda wa ADF walioshiriki mauaji hayo. Msemaji wa Misheni ya Kulinda Amani DRC, Monusco, Kanali Felix Basse alisema Umoja wa Mataifa umeongeza vikosi vya ulinzi eneo lililofanyika mauaji hayo.
“Tumepeleka askari zaidi eneo la Beni baada ya shambulio lile,” alisema Kanali Basse na kuongeza:
“Ni lazima kuendelea na mapigano haya... Nitazungumza na Waziri wa Ulinzi wa Tanzania (Dk Hussein Mwinyi), Dar es Salaam kumweleza hali ilivyokuwa na nini kinafanyika,” alisema Kanali Basse.
Hata hivyo, alisema UN haitakubali kuona suala hilo likijitokeza tena na tayari vikosi vimeongezwa katika eneo lilipotokea mauaji hayo yaliyoacha askari wengine 13 kujeruhiwa.
Baraza la Usalama lalaani
Wanachama wa Baraza la Usalama la UN, wamelaani mauaji hayo wakisema hatua hiyo inazorotesha jitihada za kuleta amani Mashariki mwa DRC.

No comments:
Post a Comment