DC MPESYA AWAMWAGIA SIFA WAFANYAKAZI MGODI WA BUZWAGI - LEKULE

Breaking

9 May 2015

DC MPESYA AWAMWAGIA SIFA WAFANYAKAZI MGODI WA BUZWAGI


Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akitoa maelezo wakati wa kumpatia zawadi za kimila, Shuka ya rubega, mkuki na ngao, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (kulia), wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye kampuni hiyo, na wengine 10 walizawadiwa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya Acacia ya tabia sita (six desired behavior), kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni pamoja na kushirikiana na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika utendaji wa kazi wa kila siku. Katika hotuba yake, Mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi, kwenye sherehe hiyo ambayo ilikuwa maalum kuwatunuku wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, na kufanyika Alhamisi usiku wa kuamkia leo Ijumaa Mei 8, 2015, aliwamwagia sifa wafanyakazi wa mgodi huo hususan uongozi mpya chini yaa Brad, kwa kuja na sera mpya ambayo sio tu inawajali wafanyakazi bali pia wananchi wanaozunguka mgodi huo ikiwemo serikali.

Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia udthabiti wa kampuni hiyo, (GM-Organizational Effectiveness), Janet Reuben-Lekashingo, (kulia), akimkabidhi cheti Isack John Nkulu, kwa utumishi wa muda mrefu kwenye kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu.

No comments: