TBL YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA SH. MIL. 22 - LEKULE

Breaking

9 May 2015

TBL YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA SH. MIL. 22


Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin akikabidhi baadhi ya vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijijicha Kambi ya Simba wilayani Karatu mkoani Arusha kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho, ambapo Kampuni hiyo ya Bia ilitoa vifaa vyenye thamani ya Sh.Milioni 22.

Mwananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ambacho ni maarufu kwa ulimaji wa zao la Shayiri akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin mara baada ya kukabidhi Kituo cha Afya cha Kijiji hicho vifaa mbalimbali vya matibabu.

Maofisa wa TBL wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo wilayani Karatu, katikati ni Afisa Uhusiano Dorris Malulu, kushoto kwake ni Mkurugenzi Jarrin na kulia kwake ni Meneja mradi wa Kilimo cha Shayiri Dk. Basson.

Afisa Uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na baadhi ya viongozi Serikali ya Kijiji pamoja na uongozi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya kituo hicho vyenye thamani ya Sh. Milioni 22, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin na kushoto kwake ni Meneja Mradi Kilimo cha Shayir Dk. Basson Bennie.

No comments: