Walcott na Sterling kubadilishana timu - LEKULE

Breaking

10 Apr 2015

Walcott na Sterling kubadilishana timu


Jarida la Starsport limebainisha kuwa Liverpool na Arsenal zinapanga makubaliano ambayo yatazifanya timu hizo mbili kubadilishana wachezaji wawili wa taifa la Uingereza.

Liverpool inahitaji pauni millioni 20 kwa nyota wake Sterling pamoja na mchezaji wa Arsenal Theo Walcot kwa mpango huo kukubalika.

Walcott angejiunga na Liverpool msimu uliopita iwapo Luis Suarez angejiunga na Arsenal.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa tayari kumuachilia Walcott kujiunga na Liverpool lakini Suarez akabadili nia na kujiunga na Barcelona.

Sasa mpango kama huo umeanza kuandaliwa huku Sterling mwenye umri wa miaka 20 akipendelea kujiunga na Arsenal naye Walcott akikosa fursa ya kuanzishwa katika kilabu ya Arsenal.

No comments: