Somalia sasa yatoa orodha ya Al Shabaab - LEKULE

Breaking

10 Apr 2015

Somalia sasa yatoa orodha ya Al Shabaab


Serikali ya Somalia imetangaza ruzuku ya dola milioni moja kwa yeyote atakayeisaidia kuwakamata viongozi 11 wa Al Shabaab.

Orodha hiyo ya watu 11 wanadaia kuwa viongozi wa ngazi ya juu ya katika kundi hilo la wapiganaji wa wa kiislamu wa Al shabaab.

Kiongozi wa kundi hilo la wapiganaji Ahmed Diriye anaongoza katika orodha hiyo huku Serikali ikitoa ruzuku ya dola laki mbili u nusu ($250,000) kwa yeyote atakayetoa habari zitakazofichua aliko.

Jumla ya dola milioni moja zimetengwa katika hatua hii ambayo inalenga kuchochea umma kuisaidia serikali hiyo kuitokomeza

kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya wanafunzi 148 wa chuo kikuu cha Garissa nchini kenya.

Orodha
Orodha ya Al Shabaab

Ahmed Diriye: $250,000 -Kiongozi
Mahad Warsame Qaley: $150,000 - Kiongozi wa Ujasusi
Ali Mohamed Raage: $100,000 - Msemaji
Abdullahi Abdi Jumaale :$100,000
Mohamed Mohamoud Nor :$100,000
Ali Mahamed Huseen :$100,000
Hasan Mahaed Ali :$100,000
Abdullahi Ismaan :$100,000
Mahamed Abdi Musa :$100,000
Mahamed Mahamuud :$100,000
Yasin Ismman :$100,000



Al Shabaab ambayo imetangaza wazi kushirikiana na wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda wameahidi kuendelea

kuishambulia Kenya hadi serikali hiyo itakapoondoa majeshi yake nchini Somalia.

Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa wanajeshi wa muungano wa Afrika .

Majeshi ya Muungano huo inashikilia maeneo mengi ya mijini kwa ushirikiano na majeshi ya Serikali ya Somalia huku

kundi hilo la Al Shabaab ikitawala maeneo ya mashambani kusini mwa taifa hilo ambalo limekuwa bila serikali kwa zaidi ya miongo miwli sasa.

No comments: