Wabunge wataka serikali kuwajibika mgomo wa wafanyabiashara - LEKULE

Breaking

1 Apr 2015

Wabunge wataka serikali kuwajibika mgomo wa wafanyabiashara

 Wabunge wameitaka Serikali kuharakisha mazungumzo yake kuhusu tatizo lililopo la mgomo wa wafanyabiashara nchi nzima, ili suala hilo lipatiwe ufumbuzi mapema.

Hayo yalibainishwa bungeni hapo na Naibu Spika Job Ndugai, wakati wakati akijibu miongozo mbalimbali iliyoombwa na wabunge kuhusu suala hilo ambao wengi wao walitaka mijadala ya Bunge hilo iahirishwe ili suala hilo lijadiliwe kama dharura.

Hata hivyo, Ndugai alisema kutokana na hali halisi iliyopo sasa ni muhimu mazungumzo hayo yakaendeshwa kwa haraka ili kufikia mwafaka na kupata ufumbuzi wa mgogoro uliopo.

Jana takribani wabunge watano, kabla ya mijadala ya miswada haijaanza kujadiliwa, waliomba mwongozo wa Spika wakitaka Serikali itoe tamko juu ya mgomo unaoendelea nchini kwa kuwa pamoja na shughuli za kiuchumi kusimama wananchi wanaatabika na kukosa huduma.

Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM), aliitaka Serikali kutoa tamko kuhusu tatizo lililopo kwa kuwa linazidi kuongezeka hasa baada ya wafanyabiashara kuongezewa kodi kwa asilimia 100, huku mwenyekiti wao, Johnson Minja, bado akiwa mahabusu.

Naye Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) alisema serikali haipaswi kulipuuzia suala hilo kwa kuwa kasi ya kusambaa kwa mgomo wa wafanyabiashara imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchi nzima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Luhaga Mpina, alisema maelezo aliyotolewa na Waziri wa Fedha yanatofautiana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wafanyabiashara walipokutana mwishoni mwa wiki.

Alisema baada ya kamati yake kubaini kuwepo kwa mgogoro baina ya Serikali na wafanyabiashara, hususani eneo la kodi na kushikiliwa kwa mwenyekiti wao Minja na mashine za EFDs, iliandaa mpango wa kukutanisha pande zote mbili kwa ajili ya kupata mwafaka.

No comments: