Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kupata fursa ya kuingia katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Yarmouk mjini Damascus, Syria.
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa ameelezea hali hiyo katika kambi ya wakimbizi 18,000 kuwa "kinyume cha ubinadamu".
Hali imezidi kuzorota tangu Aprili Mosi, wakati wapiganaji wa Islamic State walipofanya shambulizi.
Wanamgambo wa Kipalestina wanaopingana na serikali ya Syria na baadhi ya wapiganaji wa Free Syrian Army wanaongoza mapigano dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.
'Hii lazima ikomeshwe'
Mwenyekiti wa baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15, Dina Kawar, ambaye ni balozi wa Jordan katika Umoja wa Mataifa, ametoa wito wa "kuwalinda raia... Kupata misaada ya kibinadamu na msaada wa kulinda maisha".
Akiwasilisha ripoti kwenye baraza hilo, Pierre Krahenbuhl, ambaye ni kutoka shirika la Palestina la kutoa misaada la Unwra, amesema hali ni ya kukatisha tamaa zaidi kuliko ilivyokuwa".
No comments:
Post a Comment