Blair apinga kura ya maoni Uingereza - LEKULE

Breaking

7 Apr 2015

Blair apinga kura ya maoni Uingereza



Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza,Tony Blair ameingia katika kampeni za uchaguzi kwa kumshambulia waziri mkuu David Cameron, kwa ahadi yake ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu uanachama wa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, EU.

Bwana Blair amesema Bwana Cameron "ametoka nje ya agenda" kwa kuahidi kufanyika kura ya maoni na kwamba kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kunatishia nafasi ya Uingereza kama "taifa kubwa duniani"

Bwana Blair anatarajiwa kusema kuwa kiongozi wa chama chake cha Labour Ed Miliband ameonyesha"ukomavu kiuongozi" kwa kuhimili shinikizo la wanaotaka kura ya maoni kuhusu Uingereza kuendelea kuwa mwanachama wa EU au kujitoa.

Lakini Bwana Cameron amesisitiza kuwa"anaweka mbele kwanza masilahi ya nchi" kwa kutaka ifanyike kura ya maoni.

Bwana Blair alishinda uchaguzi mkuu akiwa kiongozi wa chama cha Labour mwaka 1997, 2001 na 2005, na aliachia nafasi akiwa waziri mkuu mwaka 2007.

Naibu mhariri wa masuala ya siasa wa BBC, James Landale amesema Bwana Blair tangu wakati huo kwa kiasi kikubwa amekuwa nje ya siasa za Uingereza, lakini chama cha Labour kina matumaini kwamba bado ana ushawishi mkubwa kisiasa ambao utawavuta baadhi ya wapiga kura."

No comments: