NIYONZIMA, NGASSA NA DIDA WAZAWADIWA NA TAWI LA FACEBOOK - LEKULE

Breaking

12 Apr 2015

NIYONZIMA, NGASSA NA DIDA WAZAWADIWA NA TAWI LA FACEBOOK



WACHEZAJI wa Yanga, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa na kipa Deogratius Munisi ‘Dida’ wapewa zawadi za pekee kwa kuiwezesha timu yao kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu msimu uliopita na mashabiki wa tawi la Facebook.

Wachezaji pamoja na wenzake na benchi la ufundi walikabidhiwa zawadi hizo na tawi la Facebook lenye makao yake Buguruni jijini Dar es Salaam jana baada ya kumaliza mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume Ilala.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi hizo, Mwenyekiti wa Tawi la Facebook, Josephat Sinzobakwila alisema kuwa wao kama mashabiki wanafurahi kuona timu imeshinda lakini pia wanahuzunika kuona timu imefungwa hivyo ili kuongeza morali wameamua kutoa zawadi.

“Tunahuzunika kama ninyi mnavyohuzunika mnapofungwa lakini pia tunafurahi kama ninyi mnaposhinda hivyo tumekuja hapa ili kuongeza morali kwa kuwapa zawadi hizi za saa kwa wachezaji wote na kinyango chenye picha ya mtu kwa wachezaji watatu waliofanya vizuri msimu uliopita”, alisema Sinzobakwila

Sinzobakwila alisema Ngassa alifunga mabao sita kwenye Klabu bingwa Afrika, Haruna Niyonzima amekuwa mchezaji wa kigeni aliyedumu Yanga muda mrefu kupita wengine na Dida alidaka mchezo kati yao na Azam na kufanikiwa kuifunga Azam msimu uliopita hivyo wakaona ni bora wawape zawadi za pekee ambazo ni kinyago chenye picha ya mtu pamona na mabango yenye picha zao wakiwa uwanjani.

Ukiachia zawadi ambazo ni maalum kwa Ngassa, Niyonzima na Dida kila mchezaji alipewa saa ya ukutani zenye jina lake huku ndani ikiwa na nembo ya Yanga kama ukumbusho.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi, Haruna Niyonzima alisema anawashuku mashabiki wa Facebook kwa kutambua mchango wake kwenye klabu ya Yanga na kuwaahidi kuendelea kuwapa raha lakini akawataka kufahamu kuna bahati mbaya kwa mchezaji kushindwa kufunga bao hivyo wawe wavumilivu inapotokea hali hiyo.

No comments: