Neno La Leo: Uzalendo Si Kujipaka Mwilini Rangi Ya Bendera! - LEKULE

Breaking

1 Apr 2015

Neno La Leo: Uzalendo Si Kujipaka Mwilini Rangi Ya Bendera!



Ndugu zangu,

Kwenye safu ya gazeti moja la kila Jumapili kwa lugha ya Kiingereza, mwandishi Amby Lusekelo anazungumzia sakata la Askofu Gwajima. ( Bishop Gwajima in hot soup?, Sunday News, Machi 29, 2015). Kuna mahali mwanasafu Amby Lusekelo anaandika; " Religion is the foundation of any person but then again, who are we without love for and loyalty to, country?"- Kwamba dini ni msingi wa kila mwanadamu, lakini, sisi ni nani bila upendo na uaminifu kwa nchi?

Kwa mwanadamu, Uzalendo kwa nchi uliyozaliwa si suala la kujipaka mwili mzima, rangi ya bendera ya taifa ya nchi uliyozaliwa, bali, ni mapenzi ya nchi yako kutoka kwenye kina cha moyo wako. Na kuwa mzalendo ina maana pia ya kuwa tayari kujitoa muhanga au, kutolewa kafara kwa ajili ya nchi yako.

Na imeandikwa, kuwa mbuzi wale wawili waliwekwa hadharani, mmoja akabebeshwa dhambi na kuachwa apotelee mwituni. Alikwenda na dhambi za mwanadamu. Ndio chimbuko la dhana ya scapegoat, neno la Kiingereza lenye maana ya mbuzi wa dhambi. Duniani kuna mbuzi wa dhambi na kondoo wa kafara.

Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi.

Inahusu dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.

No comments: