YANGA SC YAIFANYA VIBAYA PLATINUM YA ZIMBABWE,YAIPIGA 5-1. - LEKULE

Breaking

15 Mar 2015

YANGA SC YAIFANYA VIBAYA PLATINUM YA ZIMBABWE,YAIPIGA 5-1.

Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans, ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa kunano kombe la Shirikisho barani Afrika, leo wamefanikiwa kutoa dozi nzito kwa wapinzani wao Platinum Stars ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-1.

Katika mchezo huo ambao umechezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kunako kipindi cha kwanza kupitia kwa Salum Telela, dakika ya 28 pamoja na Haruna Niyonzima, dakika ya 44, lakini haikuchukua muda mrefu, Wazimbabwe hao wakasawazisha kufatia adhabu ndogo, ambapo walipiga faulo na mpira kuzama kimiani moja kwa moja katika dakika 45.

Licha ya kukosa mabao mengi katika kipindi cha kwanza, ambapo zaidi ya nafasi tatu za wazi washambuliaji wa Yanga walishindwa kuzitendea haki, Nyota wa Burundi, Amisi Tambwe ikiwa ni dakika ya 46 yaani dakika moja tu baada ya kipindi cha kwanza kuanza akafanikiwa kucheka na nyavu akiandika bao la tatu (3) na kuamusha morali kwa wachezaji wa Yanga.

Yanga wakizidi kushambulia kwa kasi lango la Platinum FC, ziliwachukua Dakika tano (5) tu kwa mara ya nne, Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania pamoja na klabu hiyo, Mrisho Ngassa ‘Uncle’ akaiandikia Yanga bao la 4 nakuzidi kuzamisha boti la Wazimbabwe hao.

Dakika ya 90 ‘Uncle’ Ngassa akawaning’iniza Wazimbabwe kwa kupachika bao la tano na kufanya Yanga waweze kuondoka katika Uwanja huo uliopo Temeke Jijini Dar es Salaam, wakiwa na furaha za ushindi wa magoli matano kwa moja.

Kufatia matokeo hayo, Platinum watakuwa na kibarua kizito cha kuwaondoa Yanga hapo baada ya wiki mbili kwani itawarazimu wapate ushindi wa bao 4-0 wakiwa kwao.

Mwisho.

No comments: