Wapiganaji wakiri kutekeleza mauaji Mali - LEKULE

Breaking

8 Mar 2015

Wapiganaji wakiri kutekeleza mauaji Mali

\

Kundi la wapiganaji linaloongozwa na mwanamgambo raia wa Algeria Mokhtar Belmokhtar linasema kuwa ndilo lililotekeleza shambulizi kwenye klabu ya burudani katika mji mkuu wa Mali Bamako jana jumamosi ambapo watu watano waliuawa.

Shirika moja la habari nchini Mauritania lilisema kuwa lilipokea taarifa iliyorekodiwa kutoka kwa kundi la Al-Murabitoun.



Kati ya wale waliouawa kwenye shambulizi hilo ni pamoja na raia wa Ufaransa , Ubelgi na Mali.

No comments: