Milipuko yawaua watu 50 Nigeria - LEKULE

Breaking

8 Mar 2015

Milipuko yawaua watu 50 Nigeria



Zaidi ya watu 50 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya mabomu yaliyofuatana siku ya jumamosi kwenye mji wa maiduguri ambo ndio chimbuko la Boko Haram.

Milipuko mitano ilitokea ndani ya saa moja kwenye masoko yenye shughuli nyingi pamoja na kwenye kituo cha basi.

Serikali ya Nigeria inasema kuwa boko haram wanaendesha mashambulizi hayo kwa sababu inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa jeshi.

Jeshi la Nigeria likisaidiwa na la Chad , Cameroon na Niger limejaribu kupambana na wanamgambo wa boko haram kuwaondoa kutoka ngome zao kabla ya uchaguzi ambao utafanyika baadaye mwezi huu.

No comments: