Wananchi wamlalamkia diwani kuzuia ujenzi wa barabara - LEKULE

Breaking

4 Mar 2015

Wananchi wamlalamkia diwani kuzuia ujenzi wa barabara



Wananchi wa kijiji cha kimbushikata ya machame wilayani hai mkoani  kilimanjaro  wamelalamikia hatua ya diwani wa kata hiyo kuzuia misaada inayotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani  isitumike  katika  kata  yake ukiwemo wa matengenezo ya  barabara  uliotolewa na mwenyekiti  wa taifa  wa  chadema  freeman mbowe.
ITV imetembelea kata hiyo na kuzungumza na wananchi  ambao pamoja na kumsukuru Mh.Mbowe kwa msaada huo  wa Greda la kutengeneza barabara wamelaani vikali    kitendo cha diwani huyona wameiomba serikali   kutofumbia macho vitendo vya aina hiyo.

Akizungumzia malalamiko hayo mwenyekiti wa taifa wa  chadema Mh.Freeman Mbowe ambaye pia ametembelea   kata hiyo amewataka wananchi kutokubali kugawanywa  kwa itikadi za kisiasa kwani lengo la siasa ni  kuleta maendeleo na wala sio kukwamisha maendeleo.

Hatua hiyo pia imekemewa na waziri wa ujenzi Mh.John Magufuli na mkuu wa mkoa wa kilimanjaro waliokuwa   katika ziara ya kukagua miradi ya barabara katika  mkoa wa huo.

No comments: