Waziri wa ujenzi Dr John Magufuli amewataka wanasiasa mkoani Kilimanjaro kutowachanganya wananchi kwa kuingiza siasa katika masuala ya maendeleo jambo linalochelewasha na kukwamisha maendeleo sambamba na kujenga chuki baina yao kutokana na itikadi za kisiasa jambo mbalo halina tija kwa taifa.
Kauli hiyo ya waziri Magufuli ameitoa katika eneo la masama mura wakati akizungumza na wananchi hao baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya kwa sadala masama hadi machame inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni nane nukta mbili na baada ya kuelezwa kuwa baadhi ya wanasiasa akiwemo diwani kuzuia greda la mbunge wa hai Mh Freeman Mbowe kutotengeneza barabara kwa madai kuwa hana kibali cha kufanya hivyo na kuongeza kuwa suala la maendeleo halina itikadi.
Akielezea kisa hicho kwa masikitiko mbunge wa jimbo hilo Mh Freeman Mbowe amesema ni vyema elimu ikatolewa kwa viongozi wa kisiasa kushirikiana katika nyanja za kimaendeleon bila kujali itikadi za kisiasa wala dini ili kuongeza nguvu jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama kwa upande wake ameelezea umuhimu wa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa barabara hiyo kutokana na kuwa kitovu cha kikanda cha maendeleo kutokana na mazao mengi kuzalishwa katika eneo hilo huku afisa mkuu wa wakala wa barabara nchini Bw Patrick Mfugale akisema kuwa barabara hiyo inatarajiwa kukamilika june mwaka huu na kwamba ilichelewa kukamilika kutokana na sababu zisizo za mkandarasi.
Mh Magufuli pia ametoa kiasi cha shilingi milioni tano katika kusaidia jitihada za ujenzi wa madarasa katika shule za kata hiyo ili kupata wataalamu wengi wazawa wa baadae katika sekta ya ujenzi.

No comments:
Post a Comment