Viongozi wa vyama vya siasa wa wilaya ya Mwanga wametakiwa kuendesha siasa za kistaarabu katika kuelekea utoaji maoni ya katiba inayopendekezwa, kuipigia kura na uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili kudumisha amani na utulivu uliopo katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Shayibu Ndemanga ametoa rai hiyo katika uzinduzi wa ugawaji wa nakala ya katiba hiyo kwa viongozi hao wakiwemo wa madhehebu, mashirika yasiyo ya kiserikali ya dini na taasisi wilaya ya mwanga.
Bw. Ndemanga amesema, kwa muda mrefu wilaya hiyo imekuwa na utulivu kwa sababu ya kuwepo kwa chama kimoja lakini mwaka huu matukio hayo yanakuja kukiwa na mwamko wa kisiasa na vyama vingine vya siasa vimejitokeza kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mwanga Bw. Jamhuri William amesema, nakala 6000 zitasambazwa katika vitongoji na vijiji vya wilaya hiyo na kuweka utarati utakaotumika ili kila mwananchi apate nafasi ya kuioma na kuielewa katiba hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bi. Theresia Msuya amewataka wenyeviti na vitongoji na vijiji kwenda kugawa nakala ya katiba hiyo kwa kuzingatia haki bila upendeleo au ubaguzi wa aina hiyo yo yote.
No comments:
Post a Comment