VIJANA WA JOGGING WASHEREHEKEA KUTIMIZA MWAKA MMOJA - LEKULE

Breaking

1 Mar 2015

VIJANA WA JOGGING WASHEREHEKEA KUTIMIZA MWAKA MMOJA


Keki maalumu kwa Kikundi cha Mji Mwema Jogging.

Mshauri wa Mgambo na Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Temeke, Luteni Kanali, Juma Sigambena akitoa vyeti.

Mshauri wa Mgambo na Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Temeke, Luteni Kanali, Juma Sigambena akitoa vyeti.

Msanii Dokii akipiga mnada wa mbuzi kwa ajili ya kuchangisha harambee ya Mji Mwema Jogging.

Mshauri wa klabu za jogging Kigamboni, Mshauri Barandu

Mshauri wa jogging, Mgaza Abdallah akiwa amevaa t-shirt yenye ujumbe wa kutimiza mwaka mmoja.



VIJANA mbalimbali wa klabu za mazoezi za jogging za Kigamboni jijini Dar es Salaam, leo Jumapili wamejitokeza katika kusherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Kikundi cha Mji Mwema Jogging kilichoanzishwa Machi 1, 2014 kikiwa na vijana 40 ambapo sasa kina zaidi ya vijana mia moja.

Sherehe ya maadhimisho hayo imefanyika katika viwanja vya Mji Mwema, Kigamboni, Dar na kuhudhuriwa na vikundi mbalimbali vya jogging vipatavyo 57 huku zaidi ya shilingi milioni moja zikichangwa kwa njia ya mnada.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Khalfan Salum, alisema “Tunakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za wazazi kuwazuia vijana wao, ukosefu wa ajira za kudumu, elimu mbalimbali na fedha za kufanyia miradi, tunawashukuru wadau wote waliotusaidi mpaka kufikia hapa tulipo.”

Aidha, mshauri wa Mgambo na Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Temeke, Luteni Kanali, Juma Sigambena akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, alisema “Mkuu wa Wilaya anawatakia sherehe njema na ametoa zawadi ya shilingi laki mbili ingawa amewataka muwe wema msikubali kutumiwa na watu wenye nia mbaya, serikali ya wilaya inajipanga kuwatengenezea programu maalumu ili kuwasaidia.”

No comments: