AZAM TV YAJA NA KAMPENI YA RELOADED NA VIFURUSHI VITATU VYA MWEZI - LEKULE

Breaking

1 Mar 2015

AZAM TV YAJA NA KAMPENI YA RELOADED NA VIFURUSHI VITATU VYA MWEZI




Kuanzia leo tarehe 1 March 2015 azamtv inakuletea punguzo la bei ya kisimbuzi, sasa utapata azamtv kwa shilingi 99,000!!! Hii ikijumuisha decoder,dishi na vifaa vyote pamoja na makato yote ya VAT!!
Azamtv inakupa uhuru wa kuchagua kulingana na kipato chako kwa kuzingatia hali tofauti za kiuchumi kwa Watanzania ili kuifanya iwe burudani kwa wote.

Tumewaletea vifurushi vipya vitatu vya bei vya malipo ya mwezi navyo ni:
AZAM PURE – 10,000/=
AZAM PLUS – 15,000/=
AZAM PLAY – 20,000/=
AZAM PURE – 10,000/=
Kifurushi cha Azam PURE, kitakuwa na chaneli za Azam ONE, Azam TWO, Sinema Zetu pamoja na local chaneli nyingine za hapa Tanzania, Kenya na Uganda kwa 10,000/= kwa mwezi kwa chaneli zaidi ya 20.

AZAM PLUS – 15,000/=
Kifurushi cha Azam PLUS kitakuwa na chaneli zaidi ya 50 kwa 15,000/= kwa mwezi na kitakuwa na chaneli kama zilizopo sasa, isipokuwa Fox Entertainment, FX na AMC.
AZAM PLAY – 20,000/=
Kifurushi cha Azam PLAY kitakuwa na chaneli zote, ikijumlisha Fox Entertainment, FX, AMC, Viasat Nature/History, pamoja na chaneli za klabu za Liverpool na Real Madrid, Fox Sports 2 na nyinginezo nyingi zitakazokuja siku za usoni kwa 20,000/= kwa mwezi.

Malipo ya mwezi ya sasa yakiisha, utaunganishwa moja kwa moja kwenye kifurushi cha Azam PLUS (15,000) Wateja wapya watakuwa na uwezo wa kuchagua kifurushi wanachotaka.
Kwa wateja wa sasa, malipo waliyolipa sasa yakiisha, wana uwezo wa kuchagua kifurushi wanachotaka PALE TU WATAKAPOTUPIGIA SIMU NA KUFANYA HAYO MABADILIKO, VINGINEVYO WATAENDELEA KUWA NA AZAM PLUS.

Kwa mfano, mteja kama amelipia 12,500/= tarehe 27 mwezi wa February, ikifika tarehe 26 March, atatakiwa kulipia 15,000/=. Kama anataka kuchukua kifurushi kingine, anatakiwa atufahamishe. Kama hatotufahamisha na kulipia bei ya kifurushi kingine, kwa mfano (angalia mifano miwili hapa):
1. Azam PURE 10,000/= (Ikifika tarehe 27 march atakuwa disconnected, na balance ya 10,000/= itabaki kwenye akaunti yake, kwa sababu haikuwa balance inayotosha kuendelea na Azam PLUS).
2. Azam PLAY 20,000/= (Ikifika tarehe 27 march ataendelea kuona chaneli za kifurushi cha Azam PLUS, kwa sababu akaunti yake bado ina Azam PLUS).

Mtandao wetu wa malipo hautobadilisha kifurushi automatically kwa sababu imeona umelipia bei ya kifurushi kingine na badala yake, Kama mteja amelipia kifurushi kimoja na anataka kubadilisha na kuweka kifurushi kingine, anaruhusiwa kwa masharti yafuatayo:

Asubiri mpaka kifurushi cha sasa kuisha na kisha atupigie tubadilishe kifurushi AU
Alipie kifurushi kipya leo, tutafunga kifurushi chake cha sasa na malipo yake yataishia hapo, ataanza na kifurushi kipya kwa malipo aliyofanya leo.

Yaani, kama umelipia kwa mfano 15,000/= kwa mwezi, siku 10 baadae ukataka kifurushi cha 20,000/=, utapoteza siku 20 zako zilizobaki kutimiza mwezi, kisha utalipia hiyo 20,000/= ambayo itakupeleka mwezi mwingine kuanzia leo.
Ni kama utaratibu wa mitandao ya simu, ukinunua bando ya wiki leo, baada ya siku 3 ukataka bando ya mwezi, utanunua tu, ila hawatarudisha hela ya bando ulilonunua.

Kama nilivyosema hapo awali, kifurushi ambacho wateja wote watakuwa nacho kuanzia tarehe 1 March, ni Azam PLUS. Kina chaneli kama za sasa hivi isipokuwa Fox Entertainment, FX na AMC.
Katika kutambua hili, kwamba hizi chaneli 3 zitaondolewa kwenye PLUS, chaneli hizi zitaendelea kuwepo kwenye PLUS mpaka tarehe 27 March ambapo ni mwezi mmoja kamili toka tarehe 28 February.

Hii tumeiweka hivi kama offer tu kwa wale ambao wameshalipia 12,500/= sasa hivi, kuwa na hizi chaneli. Baada ya hapo, ni 15,000/= for PLUS kama mtu anazitaka sana hizo channel za Fox Entertainment,FX na AMC anaweza kuongeza 5,000/= kupata hizo na chaneli zote nyingine kwenye kifurushi cha PLAY.

Kwa hiyo basi, kuanzia tarehe 1 March, mfumo wetu wa malipo utawaunganisha wateja wote na kifurushi cha Azam PLUS au kinyume na hapo mteja awe ameomba kifurushi kingine.
Yaani wale mlilolipia mwezi 1-2-3 na kuendelea wote kuanzia leo mmeunganishwa na kifurushi cha Azam Plus mpaka pesa mliyolipia itakapoisha na kama ikitokea unataka ubadilishwe kifurushi basi tupigie simu tutakubadilisha.

Hivyo basi, utaratibu wetu wa malipo umetengeneza mfumo mpya wa bei hizi kuanzia tarehe 1 March 2015.Hii ni muhimu sana kuielewa maana kama mtu amelipia zaidi ya mwezi leo au siku za nyuma kwa mfano, akaunti yake itakuwa na credit. Lakini tarehe ya bill yake ikifika, atapewa bill ya bei mpya.

Kwa mfano, kama mteja kalipia miezi 2 tarehe 27 February kwa shilingi 25,000/=, akaunti yake itamchaji 12,500/= hadi tarehe 26 March na atabakiwa na 12,500/= kwenye akaunti. Itakapofika tarehe 26 March atapewa bill ya 15,000/= ambayo atatakiwa kuongeza 2,500/= ili kuweza kuendelea na mwezi mwingine, vinginevyo akaunti itakuwa disconnected tarehe 27 march kama hakuongeza salio.

Hii inamaanisha kuwa channel zitafungiwa lakini pesa yako itakuwa imebakia kwenye account yako unachotakiwa kufanya ni kuongeza pesa kidogo (2500) kuendelea kutumia kifurushi hicho cha Play, au kama utataka kuhamia kifurushi kingine ndipo unatupigia simu tunakuhamisha kifurushi kwenda kile utakacho.

Tumejaribu kuelezea kwa kina kadri tuwezavyo ila kwa ufafanuzi zaidi msisite kutupigia kwa namba zetu za huduma kwa wateja
0784 108000
0764 700222
Jikoki..
Jiongeze kiburudani..
Azamtv Reloaded
Imetolewa na Mkurugenzi wa Azam Media Ltd
Rhys Torrington

No comments: