TIMU ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni imefungwa mabao 6-2 na Misri kwenye mchezo wa kutafuta kufuzu fainali za Afrika uliochezwa kwenye ufukwe wa Escape One, Dar es Salaam jana.
Tanzania iliuanza mchezo huo kipindi cha kwanza kwa kuifunga Misri mabao 2-1 yaliyofungwa na Ally Rabbi na Mwalimu Akida.
Kipindi cha pili, Misri walicharukana kuifunga Tanzania mabao matatu na kufikisha mabao 4-2 na kipindi cha mwisho wakifunga mabao mengine mawili na kufikisha mabao 6-2.
Wafungaji wa Misri ni Yehia Ally aliyefunga manne, Islam Ahmed na Mohamed Faway waliofunga bao moja kila mmoja.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Stars, John Mwansasu alisema wachezaji wake walifungwa kwa vile hawakupata muda wa kupasha mwili kutokana na kuchelewa kufika uwanjani kutokana na foleni kwani hawakuwa na polisi wa kuwasindikiza uwanjani kutoka kambini Bamba Beach, Kigamboni.
Pia alisema Misri wana uzoefu na wana uwezo wa kumiliki mpira kuliko wao ila anajiandaa kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Misri baada ya wiki moja
No comments:
Post a Comment