Serikali yatahadharisha kuhusu ugonjwa wa Dengue - LEKULE

Breaking

16 Mar 2015

Serikali yatahadharisha kuhusu ugonjwa wa Dengue

Serikali jijini Dar es Salaam imetoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa dalili za kufumuka kwa ugonjwa wa Dengue katika kipindi hiki cha mvua, huku ikiwataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama maeneo yao ili kunusuru maisha yao.

Akizangumza  na  waandishi  wa  habari  leo ,  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck  Sadiki amesema  katika kuelekea  kwenye  kipindi  cha  mvua mwezi huu magonjwa mengi hutokea kutoka na kuongezeka kwa mazalia ya mbu na uchfunzi wa mazingira hivyo wananchi wanatakiwa kujianda kwa lolote

“Hakuna mtu asiyetaka mvua, mvua ni neema na sasa tunaelekea kwenye kipindi  cha  mvua, kipindi hiki huwa  kinaambana  na   milipuko mbalimbali ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Dengue  kwa ajili  ya  maji kuhama na kutengeneza  mazingira  ya mbu, hivyo natoa wito kwa wananchi kutunza mazingira yao.” Amesema Meck Sadiki

Meck  Sadiki  ameongezea kuwa mbu anayeendeza ugonjwa huu hatari wa Dengue anapendakuishi na kuzaa kwenye maji  jaliyohifadhiwa  kwenye ndoo, mapipa , tenki, vyungu vya  maua na pindi wanapozaliana kwa wingi husababisha  maambukizi.

“Dalili za  homa ya Dengue  zinasababishwa na virusi   vinavyoambukizwa  kupitia  mbu huyu aina ya ‘aedes egptian’ na husababisha homa kali,  kuumwa kichwa , misuli na viungo mara kwa mara pia mgonjwa huwa na kichefuchefu wakati wote.”amesema Meck Sadick

Ametoa wito kwa  wananchi  kusafisha mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu, na kutangaza kuwa utupaji wa taka  ovyo ni marufuku maana hizo taka zinachangia mitaro  kuziba na maji kuhama, na kuongeza kuwa watu wote wanatakiwa kuepuka mikusanyo isiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na kuvaa nguo ndefu.

Meck  Sadiki  amewataka wananchi kutumia vyandarua vilivyo tiwa dawa na kuweka wavu na kuzuia mbu katika madirishani yao, ikiwa ni pamoja na wale wananchi wanaoishi mabondeni kuhama haraka maeneo yao kwani ni hatarishi  Zaidi kwa mazalia ya mbu.

No comments: