Kinana: Ujenzi barabara ‘ya Ngorongoro’ umeiva - LEKULE

Breaking

16 Mar 2015

Kinana: Ujenzi barabara ‘ya Ngorongoro’ umeiva

Ngorongoro. Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema mpango wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Monduli kupitia Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro hadi Mugumu umekamilika baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza mazungumzo na nchi zilizokuwa zimegoma.

Kinana alito kauli hiyo jana alipozungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wasso wilayani Ngorongoro, akisema kuwa mkutano wa Rais Kikwete na wadau uliwezesha kukubalika kwa ushawishi wake na kuondolewa na vitisho vilivyokuwa vimewekwa.

Kauli ya Kinana imekuja wakati kuna kesi imefunguliwa Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) na asasi isiyo ya kiserikali ya Africa Network For Animal Welfare (ANAW) ya Nairobi, Kenya ikipinga ujenzi wa barabara hiyo.

Katika hukumu ya jopo la majaji wa EACJ walioongozwa na Jaji Kiongozi Jean Bosco Butasi, Juni 20, 2014 Tanzania ilitakiwa kusitisha mradi wowote wa ujenzi kutokana na athari ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na utekelezaji wake.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania amekata rufaa kupinga hukumu hiyo na shauri hilo bado liko kwenye mchakato wa usikilizaji.

Kinana alisema katika mazungumzo hayo, Rais alieleza adhima yake katika ujenzi huo kuwa si kujenga barabara ya lami kwenye eneo lote, bali kilomita 50 tu ambazo ni sehemu ya mapito ya wanyama hao zitaachwa.

“Kwa sasa upo umuhimu mkubwa wa barabara hiyo ya kiwango cha lami kwa kuwa idadi ya watu wanaotumia barabara hiyo imeongezeka tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma,” alisema Kinana.

Alisema haiwezekani msimamo huo ukaendelea kushikiliwa kwa kuwa itakuwa ni sawa na kumthamini mnyama kuliko binadamu, jambo ambalo si sahihi

No comments: