Rais Kikwete amesema anajivunia hatua ambayo serikali imepiga katika kuwawezesha wanawake. - LEKULE

Breaking

9 Mar 2015

Rais Kikwete amesema anajivunia hatua ambayo serikali imepiga katika kuwawezesha wanawake.





Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema anajivunia kuona anamaliza muda wake akiwa amefanikisha kujenga msingi imara ya kuwawezesha na kuwapa nafasi wanawake katika ngazi za uongozi na hivyo kuwata viongozi wajao waendelee kuwapa fursa wanawake katika kuendeleza taifa.
Rais Kikwete ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika kitaifa katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro ambapo amesema anamaliza muda wake akiwa na amani kwa kuwa serikali imepiga hatua katika kuwaendeleza wanawake na kwa kutambua mchango wao katika ngazi ya kupunguza umasikini na kuendeleza taifa.

Aidha rais Kikwete amesema tunapofanya tathimini hakika taifa limepiga hatua na hii inajidhihirisha katika katiba inayopendekezwa na hivyo kuwataka wanawake kuunga mkono katiba hiyo ipite ili kwakua ni chombo kitakachoweza wanawake kupata haki sawa katika nyanja za siasa na uongozi.

Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Sofia Simba amesema miaka 15 tangu ulingo wa Beljin serikali imeweka kipaumbele kwa kuwezesha wanawake katika sekta mbalimbali zikiwemo nafasi za ajira na uongozi pamoja na kurekebisha vipengele vinavyokandamizi kwa wanawake nae mwakilishi wa mataifa amesema maswala ya kijinsia lazima kupewa kipaumbele kwa taifa lolote ili kuleta maendeleo.

Nao washiriki wa maadhimisho hayo kutoka taasisi mbalimbali za serikali wamesema maadhimisho hayo yalenge kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za kupata matibabu na ajira zilizo salama.

Katika maadhimisho viongozi na tasisi zilizonyesha mchangano katika kuendeleza wanawake akiwemo rais Kikwete na Spika wa mbunge la jamhuri ya muungano na mama Getrude Mongela maadhimisho hayo yamepanbwa na burudani mbalimbali ikiwemo maandmano na kisha nyimbo zilizotumbuizwa na wasanii Stara Tomas na Peter Msechu kwa kushirikiana na wafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana kilakala.

No comments: