Asilimia 30 ya wanafunzi wa kike wa sekondari za kata mkoani kilimanjaro wanapata mimba kwa kukosa mabweni ya kulala. - LEKULE

Breaking

9 Mar 2015

Asilimia 30 ya wanafunzi wa kike wa sekondari za kata mkoani kilimanjaro wanapata mimba kwa kukosa mabweni ya kulala.



Asilimia 30 ya wasichana wanaosoma sekondari za kata mkoani kilimanjaro wanapata ujauzito kabla ya kumaliza masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutembea umbali mrefu na ukosefu wa miundombinu bora pamoja na mabweni ya kulala katika shule hizo.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la kuinua wanawake kiuchumi Bi.Aginatha Rutazaa wakati wa kupokea taarifa za utafiti uliofanywa katika jamii kuhusu changamoto zinazowakabili wanawake ili zitafutiwe ufumbuzi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Amesema bado wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na mfumo dume na baadhi ya mila kandamizi ambazo zinawanyima wanake haki katika jamii.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya siha Bw.Rashid Kitambulio amesema ni vema wanaharakati wa haki za binadamu wakaelekeza nguvu maeneo ya vijijini na kutatua kero zinazowakabili wanananchi hususani wanawake na watoto.

Naye meya wa manispaa ya moshi Bw.Japhary Michael amewataka viongozi wa serikali kushirikiana na wanaharati wa haki za binadamu kuwasaidia wananchi kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika jamii.

No comments: