Picha binafsi na madhara yake - LEKULE

Breaking

23 Mar 2015

Picha binafsi na madhara yake

Wafanyakazi wawili wa kitengo cha zimamoto nchini Urusi , Ilya Bykov na Rostislav Krylov waliushangaza ulimwengu na kuwa chanzo cha gumzo mitandaoni pale walipoamua kupiga picha binafsi wakiwa wamesimama mbele ya jingo linaloteketea kwa moto huku wakiwa wamevalia mavazi ya zimamotoc,na inaarifiwa kuwa katika janga hilo la moto watu kumi na saba walipoteza maisha na ajira ya askari hao wa zimamoto iko mashakani.
Wafanya kazi hao ambao ni askari wa kitengo cha zimamoto Ilya Bykov, mwenye umri wa miaka 30,na Rostislav Krylov,mwenye umri wa miaka 28, walipata mwito kutoka katika duka liitwalo infernolililoko Kazan katikati ya Urusi jamhuri ya Tatarstan, walipofika eneo la tukio waliushangaza umati wa watu kwa kuamua kupiga picha mbele ya duka hilo kabla ya kuanza kazi rasmi ya uzimaji moto.
Moto huo uligharimu uhai wa watu wapatao kumi na saba na kuwajeruhi wengine hamsini na watano,akiwemo polisi mmoja na wafanyakazi wawili wa kitengo hicho cha dharula.
inasadikiwa chanzo cha moto huo kilianzia katika mgahawa wa jirani ambao ulitambuliwa na askari mmoja wa eneo hilo kabla ya kuwapigia kitengo hicho cha dharula cha zima moto baada ya kuona unamshinda nguvu.

Tabasamu,tupate picha nzuri
wafanya kazi hao wawili wa kitengo cha dharula,picha yao ilisambaa kwa haraka kama moto wa nyikani na kuwa gumzo kubwa katika mtandao wa kijamii wa VKontakt, kwenye kurasa za Facebook,picha inayowaonesha wanaume hao wawili wakiwa wameachia tabasamu mwanana mbele ya moto na moshi mkubwa ukiwa umezingira jingo lililokuwa likionekana nyuma yao.
Shuhuda mmoja aliye staajabishwa na tukio hilo,Yegor Tokaryev aliandika : ‘Mungu wangu, watu wanakufa hapa,na wanaume hawa wanatabasamu na kupiga picha! Na walitakiwa kuokoa maisha badala yake wana fanya haya!
Mwingine akatupia katika ukurasa wake wa facebook kuwa,nimeshangazwa na tukio hili,nashindwa kuamini,wakati wengine wakiteketea kwa moto hadi kufa,hawa wawili walikuwa wakipiga picha kama utani vile.
kwa sasa wenye mamlaka nchini Urusi wameitisha picha hizo,na huenda wakawachukulia hatua za kinidhamu wawili.
msemaji wa kitengo cha dharula nchini Urusi naye ameshangazwa na tukio la wawili hawa,kinyume na wengine ambao wakifika katika eneo la tukio hutekeleza wajibu wao tu uliowapeleka kwa ufanisi mkubwa kuokoa mali na maisha ya watu .

No comments: