PAUL MAKONDA KUTATUA MGOGORO WA UMOJA WA MAFUNDI MAGARI NA MWEKEZAJI TEGETA DAR - LEKULE

Breaking

30 Mar 2015

PAUL MAKONDA KUTATUA MGOGORO WA UMOJA WA MAFUNDI MAGARI NA MWEKEZAJI TEGETA DAR



MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ameanza kufanya juhudu za makusudi za kujaribu kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya Umoja wa Mafundi Magari Tegeta dhidi ya mmoja wa wawekezaji wilayani humo.

Jitihada hizo ameanza kuzichukua ili kujaribu kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu na kudumaza shughuli za maendeleo katika eneo hilo la mgogoro lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana na mafundi eneo la Tegeta zilipo gereji mbalimbali zinazo milikiwa na wanaumoja hao alitoa mapendekezo ya kukutana na viongozi wa umoja na mwekezaji ili kufanya mazungumzo ya pamoja kwa ajili ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo.

"Eneo hili tayari mahakama imemtambuwa mmiliki wake ambaye ndio mlalamikaji lakini hata hivyo kuna kila sababu ya kukutana na pande zote pamoja na mwekezaji huyo ili tupate ufumbuzi wa mgogoro huu ili uishe ili shughuli za maendeleo ziweze kuendelea" alisema Makonda.

Akizungumzia mgogo huo Naibu Katibu mku wa umoja huo Nationi Ndela alisema ni wa siku nyingi na kuwa kila wanapokwenda wamekuwa hawafanikiwi ambapo walimuomba mkuu huyo wa wilaya kuwasaidia.

Ndela alisema uwekezaji waliouweka katika eneo hilo unafikia zaidi ya sh.bilioni 35 hivyo ni vizuri serikali ikaliangalia jambo hilo kwa ajili ya kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa ndani.

Alisema kwamba mwekezaji anayedaiwa kumiliki eneo hilo alikuwa na kiwanda cha kutengeneza mabati aina ya asbesto na mara ya mwisho kufanya uzarishaji wa bati hizo ilikuwa kwenye miaka ya 70 tangu wakati huo eneo hilo lilikuwa wazi.

DC Makonda mbali ya kukutana na wamiliki wa gereji hizo pia alikutana na wananchi wa Bunju B Kitunda ambao nao wanamgogoro wa ardhi na mwekezaji ambapo aliwataka viongozi wa eneo hilo kufika ofisini kwake baada ya sikukuu ya pasaka ili kujua chanzo cha mgogoro huo.

Makonda ilikukabiliana na migogoro ya ardhi katika wilaya yake ameanzisha utaratibu wa kukutana na pande zinazovutana kila Ijumaa ili kuitafutia muafaka.

No comments: