MWANAHARAKATI WA WANYAMA PORI TANZANIA AMPONGEZA RAISI KENYATA - LEKULE

Breaking

5 Mar 2015

MWANAHARAKATI WA WANYAMA PORI TANZANIA AMPONGEZA RAISI KENYATA


Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Kidon Mkuu, akiwa Philipine Manila December 2014 kwenye matatembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na Susan Jaylo
Mwanaharakati Kidon Mkuu akiwa kweye hoteli alikoshukia ya Sofitel mjini Manila Philipine



Na Pamela Mollel,Arusha
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Bw.Kidon Mkuu amempongeza Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kitendo cha kuchoma moto meno ya tembo tani 15 katika kuhadhimisha siku ya wanyamapori Dunia

Bw.Mkuu aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akiongea na vyomba vya habari kuhusu siku ya wanyamapori dunia, ambapo alisema kuwa anamuunga mkono Rais huyo kwa kufanya tukio hilo la kihistoria la kuchoma meno ya tembo.

Alisema faida ya kufanya hivyo ni kudhibiti masoko na mianya ya kusafirisha meno hayo hali itakayosaidia ujangili wa tembo kupungua

Aidha alitoa wito kwa serikali na wizara kuhamasisha jamii kuhusu siku ya wanyamapori dunia kama wanavyofanya nchi zingine hali itakayosaidia jamii kufahamu wajibu wao wa kulinda wanyamapori

Siku ya Wanyamapori Duniani ilitangazwa na Baraza la Umoja wa Mataifa Desemba 20, 2013 ili kuhamasisha kulinda wanyamapori na mapori na uhadhimishwa tarehe3 April kila mwaka

No comments: