MWAKIFWAMBA KITANZINI, ATAKIWA KUACHIA NGAZI! - LEKULE

Breaking

30 Mar 2015

MWAKIFWAMBA KITANZINI, ATAKIWA KUACHIA NGAZI!



KIBANO! Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff), Simon Mwakifwamba amejikuta kwenye wakati mgumu kwenye mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika kwenye ofisi za shirikisho zilizopo Kinondoni, Dar akitakiwa kuachia ngazi.
Habari kutoka kwa sosi aliyekuwa ndani ya kikao hicho zilinyetisha kwamba, wanachama wa shirikisho hilo walisema wamechoshwa na rais huyo na kwa sababu muda wake umekwisha, alitakiwa kuachia ngazi.

Mwakifwamba amebanwa sana, ametakiwa kuachia ngazi na kueleza amefanya nini kwenye uongozi wake ikiwa ni pamoja na kueleza gari la shirikisho amelipeleka wapi kwani tangu apate nalo ajali hata katibu wake hajui limekwenda wapi,” alisema sosi huyo.
Baada ya habari hizo kutua kwenye meza ya Ijumaa Wikienda, mwanahabari wetu alifika ofisini kwa Mwakifwamba na kukuta kikao kikiendelea.


Baada ya kikao hicho mwandishi wetu alipata fursa ya kuzungumza na Mwakifwamba ambaye alikiri kuulizwa kuhusiana na gari ambapo aliwaambia lipo gereji.

No comments: