Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yupo tayari kufa kwa kutetea misingi ya haki na utawala wa sheria katika kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
Alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Bustanini, Kiembesamaki, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika mkutano ambao waziri wa zamani wa SMZ, Mansour Yussuf Himid aliutumia kutangaza kugombea uwakilishi katika jimbo hilo.
Maalim Seif alisema tayari Jeshi la Polisi limeanza kuweka mizengwe katika upatikanaji wa viwanja vya mikutano ya hadhara kwa madhumuni ya kuibeba CCM, jambo ambalo halikubaliki kwa kuzingatia misingi ya demokrasia.
Alisema kitendo cha Polisi Wilaya ya Magharibi kuzuia Uwanja wa Baraza la Wawakilishi ambao ulipangwa kutumika kwa mkutano huo kinaonyesha kuwa baadhi ya watendaji wa jeshi hilo bado hawajabadilika.
“Nakwambieni safari hii kama polisi mmeleta mabomu ya kupiga watu wakati huu wa kuelekea uchaguzi, basi safari hii mtamuua Makamu wa Kwanza wa Rais, sitakubali kuona haki na misingi ya utawala wa sheria ikivunjwa,” alisema Maalim Seif.
Alisema mikutano ya vyama vya siasa inasimamiwa na Sheria namba tano ya Vyama vya Siasa, lakini masheha na viongozi wa wilaya wamekuwa kikwazo kwa mikutano ya wapinzani kufanyika, jambo ambalo ni kinyume na misingi ya demokrasia.
Kuhusu Mansour
Alisema Mansour ni kiongozi mwenye dira na uchungu wa kweli wa kuwatumikia wananchi na kulinda haki za Zanzibar.
Akihutubia katika mkutano huo, Mansour alisema atatumia nguvu zake zote kufanya kampeni nyumba kwa nyumba, tawi kwa tawi, hadi jimbo hilo alitie mikononi.
“Sitoona haya kuingia tawi kwa tawi kusaka kura kwa ajili ya CUF, matawi yote ya CCM katika jimbo hili nimeyajenga mwenyewe nitafanya kampeni za nyumba kwa nyumba na sina kinyongo na kufukuzwa CCM,” alisema.
Alikumbushia kukamatwa kwake na Jeshi la Polisi na kufunguliwa kesi ya kupatikana na risasi kinyume na sheria na kuwataka wananchi wa Zanzibar kuacha kushabikia mambo yanayokwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Alisema Zanzibar imepita katika misukosuko mingi na kuwataka wananchi kuendelea kulinda na kuthamini misingi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo imesaidia kupunguza chuki.
Viongozi wengine waliohutubia katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya maridhiano, Hassan Nassor Moyo, ni Mwakilishi wa Mjimkongwe Ismail Jussa Ladhu, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Salim Bimani na naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui.

No comments:
Post a Comment